• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 29, 2013

  ETO'O ATUA KWA 'GOGO' LONDON TAYARI KUKAMILISHA USAJILI WAKE CHELSEA

  IMEWEKWA AGOSTI 29, 2013 SAA 12:42 ASUBUHI
  KLABU ya Chelsea itamsaini Samuel Eto’o kwa Mshahara wa Pauni Milioni 7 kwa mwaka leo Alhamisi baada ya kukubali matokeo ya kumkosa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
  Eto’o, mshambuliaji wa Cameroon mwenye umri wa miaka 32 amekubali malipo hayo kidogo kutoka Pauni Milioni 17 alizokuwa akilipwa Anzhi Makhachkala kwa mwaka na kumfanya awe mchezaji anayelipwa zaidi duniani na atasaini kama mchezaji huru.
  Pamoja na hayo, inafahamika Anzhi imemlipa mamilioni Eto’o ya Pauni ili kuvunja naye Mkataba.
  Full steam ahead: Samuel Eto'o arrived at St Pancras station on Wednesday night ahead of his move to Chelsea
  Kifaa kinawasili: Samuel Eto'o akiwasili Stesheni ya Treni ya St Pancras jana usiku tayari kukamilisha uhamisho wake Chelsea
  Whisked away: Eto'o leaves St Pancras after arriving in London
  Whisked away: Eto'o leaves St Pancras after arriving in London
  Ndani ya Treni: Eto'o, anayetarajiwa kupata mshahara wa chini Chelsea, akiwa ndani ya Treni baada ya kutua St Pancras jana usiku
  Solution? Samuel Eto'o will seal his move to Chelsea as Jose Mourinho ends his striker search
  Suluhisho? Samuel Eto'o anatua Chelsea kumaliza tatizo la safu ya ushambuliaji kwa Jose Mourinho
  Top target: Mourinho didn't select any strikers at Old Trafford and is known to be chasing Wayne Rooney
  Mlengwa: Mourinho amemkosa Wayne Rooney wa Man United

  REKODI ZA MAGWIJI CHELSEA KABLA YA SAMUEL ETO'O

  Chelsea imewahi kusaini wachezaji wakongwe kabla ya Eto'o na imepata matokeo tofauti. . .
  George Weah
  Mchezaji bora zaidi daima Afrika alitua mwaka 2000 kutoka AC Milan, akiwa na umri wa miaka 33. Hakupewa nafasi sana chini ya kocha Gianluca Vialli, licha ya kufunga bao katika mchezo wake wa kwanza na Spurs. 
  MATOKEO: Alifeli.
  Gianfranco Zola
  Alitua London mwaka 1996 akiwa na umri wa miaka 30 na katika mechi 312 alifunga mabao 80, na kujitengenezea heshima kubwa darajani.
  MATOKEO: Alifanikiwa.
  Gianluca Vialli
  Akiwa na umri wa miaka 32-alikataa kujiunga na Rangers na kusaini kikosi cha Ruud Gullit mwaka 1996. Lilikuwa dau kubwa la Pauni 600,000 na Vialli akaenda kufunga mabao 40 katika mechi 78, kisha akaeukia kuwa kocha mwenye mafanikio. 
  MATOKEO: Alifanikiwa.
  Pop Robson
  Gwiji huyo wa Newcastle na West Ham alijiunga na Chelsea akiwa na umri wa miaka 36 mwaka 1982. Alifunga katika mechi yake ya kwanza, lakini akafunga mabao mawili tu zaidi akiwa kocha na mchezaji. 
  MATOKEO: Alifeli.
  Andriy Shevchenko
  Milan ilisikitika wakati Sheva anaondoka akitimiza miaka 30 kwa dau la Pauni Milioni 30.8. Lakini mashabiki wa Chelsea muda si mrefu walijutia usajili wa mshambuliaji huyo wa Ukraine, ambaye aliishia kufunga mabao 22 katika misimu mitatu.
  MATOKEO: Alifeli.
  Eto'o aliwasili katika Stesheni ya Treni ya London, St Pancras usiku wa jana na anatarajiwa kufanyiwa vipimo katika viwanja vya mazoezi vya Chelsea, Cobham kabla ya kukamilisha usajili wake leo.
  Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, alithibitisha kumfanya Eto’o mchezaji wa pili anayemzikia na mpango wake B baada ya United kugoma kumuuza Rooney.
  Kwa sasa, mshambuliaji huyo wa England ameamua kuendelea na maisha Old Trafford baada ya kuandika katika ukurasa wake wa Facebook kuwashukuru mashabiki kwa mapokezi mazuri wakati United ikimenyana na Chelsea na kutoa sare ya bila kufungana usiku wa Jumatatu.
  Rooney aliposti: "Ilikuwa vigumu kuamini namna mashabiki walivyofanya, nawashukuru mno. Hakika nakubali sapoti yenu. Inamaanisha mengi,".
  Mourinho anaweza kujaribu tena baadaye msimu huu kuinasa saini ya Rooney, lakini kwa sasa anamaliza shida zake kwa Eto’o, ambaye aliwahi kumzungumzia kwamba: "Kocha yeyote atakuwa mpumbavu kutotaka kuwa na mshambuliaji kama yeye,".
  Kuna mambo makubwa yanatarajiwa kutokana na kocha huyo wa Chelsea na mchezaji wake huyo mpya.
  Eto’o hajawahi kwenda tofauti na matarajio. Akiwa Barcelona, alikamata kipaza sauti katika matangazo ya moja kwa moja ya Televisheni na kuikandia klabu yake ya zamani, Real Madrid ‘b*****ds’ kushangilia taji la Barcelona la ubingwa wa Hispania mwaka 2005; aliwahi pia kuponda hadharani kiwango cha chini cha Ronaldinho na aliwahi kuondoka uwanjani baada ya mashabiki jukwaani kuanza kumfanyia hila za kibaguzi katika mechi na Zaragoza.
  Ajabu pamoja na urafiki wake na Mourinho kwa sasa, lakini wametokea kuwa adui kiaina fulani.
  Alipokwenda Stamford Bridge mwaka 2005 wakati Chelsea ilipoifunga Barcelona katika Ligi ya Mabingwa, Eto’o alitoa maoni yake akikandia mbinu za kiuchezaji za Chelsea. Mourinho anapenda uimara wa mchezaji huyo.
  "Nilipenda ukweli kwamba anafanya kazi kwa kujituma,"alisema Mourinho.
  Wawili hao baadaye waliuangana Inter Milan ambako Eto’o alimuwezesha Mourinho kushinda mataji matatu ndani ya msimu. Wakati huo, Mwanasoka huyo bora mara nne Afrika alifunga bao pekee la ushindi Stamford Bridge na kumaliza matumaini ya Chelsea katika Ligi ya Mabingwa.
  Reunion: Eto'o and Mourinho won the treble at Inter Milan in 2010
  Wanaungana tena: Eto'o na Mourinho walitwaa mataji matatu Inter Milan mwaka 2010
  Treble
  Maswali tu ni kwamba bado ana kasi ile ile iliyomfanya tishio kwa wapinzani Italia na Hispania na kulikuwa kuna ushahidi mwaka jana katika Ligi ya Urusi na Ulaya, Europa League kwamba kasi yake inapungua sambamba na kuongezeka kwa umri wake.
  Pamoja na hayo, shaka juu ya kasi yake inaondolewa na uhusiano wake na mchezaji mpya mwingine wa Chelsea kutoka Anzhi, Mbrazil Willian, ambao umekuwa ukizalisha mabao japo moja katika mechi mbuili. Ni bahati nasibu Mourinho anacheza kumsajili Eto’o.
  "Kuna Jose Mourinho mmoja tu," Eto’o aliwahi kusema wakati fulani juu ya kocha wake huyo wa zamani. "Nimecheza chini ya makocha wengi wakubwa, lakini hakuna mtu mfano wa Jose katika katika mchezo huu,". 
  defeat: The signing effectively kills any hope Mourinho had of signing United striker Rooney
  Pio: Mourinho amemkosa mshambuliaji wa United, Rooney
  Writing's on the wall: Wayne Rooney took to Facebook to thank Old Trafford fans on Monday night
  Alichoandika kwenye ukurasa wake: Wayne Rooney ametumia ukurasa wake wa Facebook kuwashukuru mashabiki wa Old Trafford kwa sapoti waliyompa kwenye mechi dhidi ya Chelsea

  "Ningependa kupata nafasi ya kucheza chini yake tena, kwa sababu haijawahi kuboa napokuwa karibu na Jose,".
  Kutua kwa Eto’o ni kama pigo kwa washambuliaji wa tatu wa timu hiyo ya Stamford Bridge. Fernando Torres na Romelu Lukaku walikuwa benchi Old Trafford usiku wa Jumatatu na Demba Ba, anayetakiwa kurejea Newcastle na kocha Alan Pardew, hakuwamo kabisa kikosini.
  Kutua kwa Willian na Eto’o haiwezi kuwa dalili za Chelsea kumaliza kununua wachezaji, kwani klabu hiyo pia ipo kwenye mazungumzo na Porto juu ya Christian Atsu, winga mwenye thamani ya Pauni Milioni 4, ambaye pia aliwahi kutakiwa na Cardiff, Tottenham na Liverpool. Na mchezaji huyo wa timu ya taifa ya Ghana chini ya umri wa miaka 21 kuna matumaini makubwa akaungana na magwiji wa Chelsea.
  Lakini iwapo watafanikiwa kumsaini Atsu mbele ya Spurs walioamua kumwaga fedha sokoni, litakuwa pigo la pili kwa Andre Villas-Boas majira haya ya joto, kufuatia kuzidiwa kete kwa Willian.
  All in blue: The Brazilian will wear the No 22 shirt
  Wote tabasamu: Kiungo wa Brazil, Willian amefurahia kukamilisha usajili wake Stamford Bridge
  Willian at Chelsea

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ETO'O ATUA KWA 'GOGO' LONDON TAYARI KUKAMILISHA USAJILI WAKE CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top