• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 20, 2013

  RUFAA YA WAPINZANI WA ARSENAL KUSIKILIZWA SIKU YA MECHI...GUNNERS YAWEZA KUSONGA MBELE HATA IKITOLEWA

  IMEWEKWA AGOSTI 20, 2013 SAA 2:56 ASUBUHI
  USIKILIZWAJI wa rufaa ya Fenerbahce kupinga kufungiwa miaka miwili kwenye michuano ya Ulaya utafanyika siku ile ile wanacheza na Arsenal mechi ya kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  Timu za Uturuki, Fenerbahce na Besiktas, ambazo  zilikutwa na hatia ya kupanga matokeo, zimekatia rufaa uamuzi wa UEFA kwa Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS).
  Taarifa kwenye tovuti ya CAS, imesema: "Usikilizwaji wa kesi ya Besiktas JK utafanyika Agosti 20, 2013 na usikilizwaji wa kesi ya Fenerbahce SK utafanyika Agosti 21 na 22, 2013 mjini Lausanne. 
  In for long? Fenerbahce's Moussa Sow scored in their qualifying round tie against Salzburg
  Watapona? Mshambuliaji wa Fenerbahce, Moussa Sow alifunga katika hatua ya mchujo dhidi ya Salzburg
  "CAS inataraji kutoa uamuzi wa kesi hizoAgosti 28, 2013 (Fenerbahce) na Agosti 30, 2013 (Besiktas).'
  Wakati droo inatangazwa, Msemaji wa UEFA alisema bado hawajaamu nini kitatokea iwapo Fenerbahce itashinda na kisha kutolewa katika Ligi ya Mabingwa.
  Mechi ya marudiano dhidi ya Arsenal itachezwaAgosti 27, siku moja kabla ya kutangazwa kwa uamuzi wa rufaa yao.
  Needing a win: Olivier Giroud will hope to grab another goal in the Champions League play-off
  Wanataka ushindi: Olivier Giroud atatumai kufunga tena katika mchezo wa kuwania kuingia kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa
  Pensive: Arsene Wenger will be wanting a better performance from his team this season
  Tafakari: Arsene Wenger atataka mchezo mzuri kwa timu yake msimu huu
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: RUFAA YA WAPINZANI WA ARSENAL KUSIKILIZWA SIKU YA MECHI...GUNNERS YAWEZA KUSONGA MBELE HATA IKITOLEWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top