• HABARI MPYA

    Saturday, August 17, 2013

    TATA MARTINO AWAPUUZA LUIZ NA AGGER, ASEMA BARCA INA UKUTA WA MAANA TU

    IMEWEKWA AGOSTI 17, 2013 SAA 9:38 ALASIRI
    KOCHA wa Barcelona, Tata Martino amepuuza taarifa za mpango wa kuwasajili David Luiz au Daniel Agger, kwa kuthibitisha anafuarahia  safu ya sasa ya ulinzi.
    Vigogo hao wa Katalunya wamekuwa wakihusishwa kutaka kuwasajili kwa fedha nyingi wachezaji hao wa klabu za Ligi Kuu England, Chelsea na Liverpool.
    Na kocha huyo mpya amesema katika Mkutano na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wake wa kwanza wa La Liga dhidi ya Levante: "Tuna Puyol, Pique, Mascherano, Bartra, pia Adriano. Ikiwa kuna majeruhi yeyote, usajili wa Januari utakuja miezi michache ijayo,".
    VIDEO Kaangalia Martino akirithi mikoba ya Vilanova Barcelona
    Not needed: Barcelona were thought to be chasing a centre-back this summer, with David Luiz (above) and Daniel Agger top of the list
    Hahitajiki: Barcelona ilifikiriwa kutaka kusajili beki wa kati majira haya ya joto na David Luiz (juu) na Daniel Agger walitajwa kuwamo kwenye orodha ya wanaotakiwa
    Not needed: Barcelona were thought to be chasing a centre-back this summer, with David Luiz (above) and Daniel Agger top of the list
    Klabu hiyo ya Hispania ilisumbuliwa na tatizo la majeruhi msimu uliopita, iliyowaponza kuchapwa 7-0 katika Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa na Bayern Munich.
    Lakini kauli ya kocha mpya inamaanisha makocha wenzake, Brendan Rodgers na Jose Mourinho wanaweza kutuliza presha zao.
    Rodgers amempa Agger Unahodha Msaidizi katika kumshawishi abaki Anfield, wakati Mourinho alisema kuhusu Luiz: "Tunataka kumbakiza na tunafahamu kwamba klabu kubwa kama Barcelona wanataka kilicho bora na wanajaribu kupata moja kati ya mabeki bora wa kati duniani, lakini tumekuwa wazi sana kwa kusema kwamba hakuna nafasi ya David Luiz kuondoka,".
    Expectant: Tata Martino speaks to the media ahead of his first competitive game in charge of Barca
    Mambo hadharani: Tata Martino akizungumza na Waandishi wa Habari kuelekea mchezo wake wa kwanza wa mashindano tangu aanze kazi Barca
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: TATA MARTINO AWAPUUZA LUIZ NA AGGER, ASEMA BARCA INA UKUTA WA MAANA TU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top