• HABARI MPYA

    Saturday, August 24, 2013

    YANGA YAANZA LIGI KWA KISHINDO, YAUA 5-1, TEGETE APIGA MBILI

    Na Zaituni Kibwana, IMEWEKWA AGOSTI 24, 2013 SAA 12:02 JIONI
    MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Yana SC wameanza vema kampeni za kutetea taji lao, baada ya kuwafumua Ashanti United ‘Watoto wa Jiji’ mabao 5-1 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Mabao ya Yanga leo yalifungwa na Jerry Tegete dakika za 10 na 57, Simon Msuva dakika ya 47, Haruna Niyonzima dakika ya 73 na Nizar Khalfan dakika ya 90, wakati bao pekee la Ashanti lilifungwa na Shaaban Juma dakika ya 89.
    Shujaa; Tegete amefunga mawili leo Yana ikiua 4-0 katika mchezo wa ufunguzi Ligi Kuu


    Tegete alifunga bao la kwanza baada ya kupokea pasi ya nyota wa mchezo wa leo, Simon Msuva na kumlamba chenga beki Tumba Sued kabla ya kumtungua kipa Ibrahim Abdallah na lingine alifunga kwa krosi ya Msuva tena na kumvuta kipa kutoka langoni kabla ya kufunga.
    Msuva alifunga bao bora zaidi katika mchezo huo, baada ya kuwalamba chenga mabeki wawili wa Ashanti, Tumba Sued na Ramadhani Malima kisha kuutumbukiza mpira kimiani kwa kichwa. 
    Niyonzima alifunga kwa kichwa akiunganisha mpira wa adhabu uliopigwa na beki David Luhende na Nizar alifunga kwa krosi ya Frank Domayo wakati Juma aliipatia Ashanti bao la kufutia machozi baada ya kuwatoka mabeki wa Yanga. 
    Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, David Luhende, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Mbuyu Twite, Athumani Iddi ‘Chuji’/Frank Domayo dk18, Simon Msuva, Salum Telela, Didier Kavumbangu/Hussein Javu dk67, Jerry Tegete na Haruna Niyonzima. 
    Ashanti; Ibrahim Abdallah, Khan Usimba, Emanuel Kichiba, Ramadhani Malima, Tumba Sued, Emanuel Memba, Fakih Hakika, Mussa Nampaka/Laurent Mugia dk61, Hussein Sued, Mussa Kanyaga/Shaaban Juma dk49 na Joseph Mahundi. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: YANGA YAANZA LIGI KWA KISHINDO, YAUA 5-1, TEGETE APIGA MBILI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top