• HABARI MPYA

  Jumatano, Agosti 28, 2013

  ETO'O KUTUA CHELSEA NDANI YA SAA 48...MOURINHO ANAMKUBALI KULIKO WOTE TORRES, BA NA LUKAKU

  IMEWEKWA AGOSTI 28, 2013 SAA 1:15 ASUBUHI
  KLABU ya Chelsea iko katika hatua za mwishoni za kukamilisha usajili wa Samuel Eto'o kutoka Anzhi Makhachkala na dili hilo linaweza kukamilika ndani ya saa 48.
  Tayari wamekwishamsajili Willian kutoka Anzhi ambaye anasubiri kibali cha kufanya kazi leo na usajili wa Eto'o utakuwa sehemu ya Pauni Milioni 32 zilizotengwa.
  Mkataba wa mshambuliaji huyo wa Cameroon utakuwa mfupi tu wa mwaka mmoja.
  Chelsea bound: Samuel Eto'o may reunite with Jose Mourinho who managed him at Inter Milan
  Kifaa cha Chelsea: Samuel Eto'o anaweza kuungana na Jose Mourinho aliyekuwa kocha wake Inter Milan
  Eto'o alianzia soka yake Ulaya katika klabu ya Real Madrid, lakini alicheza mechi tatu tu na akapelekwa kwa mkopo katika miaka yake minne na klabu hiyo ya Jiji la Hispania.
  Alitengeneza jina alipokuwa akichezea Mallorca kabla ya kusajiliwa na Barcelona. Aliiwezesha kushinda Ligi ya Mabingwa, akifunga dhidi ya Arsenal katika Fainali mwaka 2006.
  Baadaye akaenda kuungana na Jose Mourinho Inter Milan, na hiyo inaweza kuwa sababu moja ya kuchaua kutua Chelsea. Kocha huyo Mreno anaweza kuwa na imani naye zaidi kuliko washambuliaji wake wa sasa, Fernando Torres, Romelu Lukaku au Demba Ba.
  Forward power: Eto'o should complete his deal to Stamford Bridge in the next two days
  Mshambuliaji wa nguvu: Eto'o anaweza kukamilisha uhamisho wake kutua Stamford Bridge ndani ya siku mbili hizi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: ETO'O KUTUA CHELSEA NDANI YA SAA 48...MOURINHO ANAMKUBALI KULIKO WOTE TORRES, BA NA LUKAKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top