• HABARI MPYA

  Jumanne, Agosti 27, 2013

  MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA RHINO KESHO, BOCCO NJE, KARIHE NA NYONI 'TIA TIA MAJI'

  IMEWEKWA AGOSTI 27, 2013 SAA 11:48 JIONI
  Kocha Mkuu wa Azam FC, Muingereza Stewart John Hall akimpa maelekezo mchezaji wake, kiungo Khamis Mcha 'Vialli' kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi mjini Tabora jioni ya leo. Azam itamenyana na wenyeji Rhino Rangers kesho kwenye Uwanja huo katika mfululizo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. 

  Mshambuliaji Seif Abdallah Karihe akitibiwa na daktari wa timu, Vincent Madege baada ya kuumia kifundo cha mguu mazoezini leo

  Beki Erasto Nyoni akipewa mazoezi mepesi na Dk, Madege leo

  Kikao cha dharula; Kocha Stewart Hall akijadiliana na wasaidizi wake Ibrahim Shikanda kulia na Kali Ongala kushoto wakati wa mazoezi leo

  Beki Agrey Morris kulia akimtoka mshambuliaji Kipre Tchetche mazoezini leo

  Beki David Mwantika akimtoka Khamis Mcha Vialli nyuma yake. Wengine nyuma ni Waziri Salum na kulia ni Jabir Aziz

  Injini ya timu; Salum Abubakar 'Sure Boy' yuko fiti kabisa kwa mchezo wa kesho

  Mlinzi Mkuu; Beki wa kati Aggrey Morris yuko tayari kwa shughuli ya maafande wa JWTZ kesho

  Jabir Aziz kushoto akiwania mpira na Mudathir Yahya

  Kocha Msaidizi, Kali Ongala alishiriki mazoezi 

  John Bocco 'Adebayor' alikuwa nje kabisa akipiga stori na Meneja Jemadari Said kwa sababu ya maumivu

  Himid Mao akijimwagia maji mazoezini leo

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MAZOEZI YA MWISHO AZAM FC KABLA YA KUIVAA RHINO KESHO, BOCCO NJE, KARIHE NA NYONI 'TIA TIA MAJI' Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top