• HABARI MPYA

  Alhamisi, Agosti 22, 2013

  IVANOVIC AEPUKA RUNGU LA FA BAADA YA KUMCHEZEA RAFU BENTEKE JANA

  IMEWEKWA AGOSTI 22, 2013 SAA 9:50 ALASIRI
  BEKI wa Chelsea, Branislav Ivanovic hatakutana na adhabu zaidi kwa rafu aliyomchezea Christian Benteke jana usiku katika mchezo wa Ligi Kuu ya England dhidi ya Astin Villa. 
  Kocha wa Aston Villa, Paul Lambert 'alimuwakia' refa Kevin Friend kwa kutomtoa beki huyo baada ya rafu hiyo mbaya, kiasi cha sekunde tu kabla hajaifungia wenyeji bao la ushindi Uwanja wa Stamford Bridge. 
  Lakini kwa sababu, Friend alimuonyesha kadi ya njano beki huyo Mserbia baada ya kuona tukio alilomfanyia Benteke, Chama cha Soka (FA ) hakitachukua hatua zaidi.
  VIDEO Kaangalie tukio la mchezaji wa timu ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Chile alivyochezewa rafu
  Villain to hero: Branislav Ivanovic elbowed Christian Benteke before scoring the winner (below)
  Kazi kazi: Branislav Ivanovic alivyomtenda Christian Benteke kabla hajaifungia Chelsea bao la ushindi
  Branislav Ivanovic scores for Chelsea
  Lambert, ambaye baada ya mechi alilalamika timu yake kuonewa katika mechi hiyo, alisema: "Nafikiri Ivanovic alicheza rafu. Nafahamu ni mchezo wa maguvu. Lakini hicho ndicho nachofikiria,".
  Mourinho, pamoja na hayo, alipuuza madai hayo akisema: "Hii soka soka ya England. Kwa sababu fulani, dunia inaipenda hii kuliko ligi yoyote,".
  Sheria za FA zimebadilika majira ya joto kufuatai tukio kama hili lililomhusisha mchezaji wa Wigan, Callum McManaman aliyenusurika adhabu kwa kumchezea rafu mchezaji wa Newcastle, Massadio Haidara. 
  Pamoja na hayo, waliamua kwamba, FA inaweza kuchukua hatua, tu iwapo refa hakuona tukio vyema.  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: IVANOVIC AEPUKA RUNGU LA FA BAADA YA KUMCHEZEA RAFU BENTEKE JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top