• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 23, 2013

  WILSHERE ATIKISA KIBERTIKI ARSENAL...ASEMA ATAONDOKA WENGER AKIFUKUZWA

  IMEWEKWA AOSTI 23, 2013 SAA 5:52 USIKU
  KIUNGO Jack Wilshere amkandia wanaomponda Arsene Wenger na kusema atafikiria mustakabali wake Arsenal iwapo Mfaransa huyo ataondoka klabuni.
  Wenger amejikuta katika wakati mgumu The Gunners kwa kutosajili huku akiwakosa wachezaji aliowataka Gonzalo Higuain, Wayne Rooney, Luis Suarez na Luiz Gustavo.
  Kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Aston Villa Jumamosi iliyopita kimesababisha mashabiki wa Arsenal, waitwao Supporters' Trust kusema kwamba itakuwa vibaya kwa bodi kumpa Mkataba mpya asiposajili hadi dirisha likafungwa.
  Jack Wilshere
  Arsene Wenger
  Onyo: Jack Wilshere amesema ataangalia upya mustakabali wake Arsenal ikiwa Arsene Wenger ataondoka
  Critics: Wilshere has also hit out at Wenger's critics, branding them 'ridiculous'
  Mgogoro: Wilshere ameponda kulaumiwa kwa Wenger

  Wilshere, pamoja na hayo amesema kwamba atalazimika kuondoka Uwanja wa Emirates kama Wenger akiondoka.
  "Nataka kushinda vitu na Arsenal na ninataka kuwapo huko muda mrefu, lakini ikiwa kocha ataondoka, mambo yatabadilika," alisema Wilshere akizungumza na Zapsportz.com.
  "Arsenal ipo moyoni mwangu wakati wote na kwa kusaini Mkataba kwa miaka mingine mitano inaonyesha ni jinsi gani nimeshikamana nao na ni wajibu wao kuniwekea kila kitu vizuri.
  Preparation: Arsenal face Fulham at Craven Cottage at lunchtime on Saturday
  Maandalizi: Arsenal itamenyana na Fulham Uwanja wa Craven Cottage mchana wa Jumamosi

  "Arsene Wenger amekuwapo kwa miaka mingi na wakati wote ameshinda mataji. Sawa, tumeporomoka mno kwa miaka mitano au sita iliyopita, lakini ni kocha babu kubwa na watu ambao wanahoji uwezo wake ni wapuuzi.
  "Amefuzu Ligi  ya Mabingwa kwa miaka 16, hivyo nafikiri ni mtu sahihi kazini,".alisema.
  Wenger aliiongoza Arsenal Jumatano usiku kuichapa mabao 3-0 Fenerbahce nchini Uturuki, matokeo ambayo yanaiweka timu katika nafasi ya kufuzu kwenye hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa.
  Miaka nane imepita sasa tangu The Gunners imeshinda taji na Wilshere ameanzisha kampeni za kumkingia kifua kocha wake.
  Another year: Arsenal's win in Turkey has virtually guaranteed their passage into the group stage of the Champions League for another year
  Mwaka mwingine: Ushindi wa Arsenal Uturuki unaiweka timu katika nafasi ya kufuzu tena hatua ya makundi ya Lii ya Mabingwa

  "Tumepoteza majina machache ya wachezaji wa nguvu miaka ya karibuni na hiyo ni ngumu kwa klabu yoyote,"alisema kiungo huyo mwenye umri wa miaka 21 wa England.
  "Kwanza tulimpoteza Thierry Henry na kisha Cesc Fabregas, Samir Nasri na Robin van Persie. "Hiyo ni ngumu, hususan wakati Robin alipohamia kwa timu nyingine England, inatupa ugumu wa kushindana.
  "Lakini sasa tumepata damu changa ya wachezaji wa England wanaoibuka na kama tutakaa pamoja na kujenga kitu, kisha tutashinda mataji katika miaka michache ijayo,".
  Losses: Selling the likes of Robin van Persie, Cesc Fabregas and Thierry Henry has made it difficult for Arsenal, says Wilshere
  Impoteza: Kuuza nyota kama Robin van Persie, Cesc Fabregas na Thierry Henry kumesababisha ugumu Arsenal, amesema Wilshere
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: WILSHERE ATIKISA KIBERTIKI ARSENAL...ASEMA ATAONDOKA WENGER AKIFUKUZWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top