• HABARI MPYA

  Jumapili, Agosti 25, 2013

  BALE ATUA HISPANIA KUKAMILISHA USAJILI WAKE WA REKODI YA DUNIA REAL MADRID

  IMEWEKWA AGOSTI 25, 2013 SAA 7:19 USIKU
  NYOTA Gareth Bale amewasili Hispania kujiandaa kusaini Real Madrid, lakini Tottenham na vigogo hao wa Hispania bado wanavutana kwenye bei.
  Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales mwenye umri wa miaka 24 alitua Malaga kwa ndege binasfi na kwenda kwa teksi hadi Marbella, ambako anatarajiwa kukaa kwa ajili ya kukamilisha majadiliano dakika za mwisho kabla ya kufungwa kwa pazia la usajili.
  PICTURE EXCLUSIVE: Bale leaves his house earlier in Essex on Friday morning as his world-record £94million move from Tottenham to Real Madrid moves closer
  PICHA YA KIPEKEE: Bale akiondoka nyumbani kwake Essex Ijumaa asubuhi kuelekea kukamilisha uhamisho wake wa kuvunja rekodi ya dunia kutoka Tottenham kutua Real Madrid

  Inafahamika Real imeweka mezani kwa ajili ya Bale Bale, Euro Milioni 100 (sawa na Pauni Milioni 86) ikijumuisha na malipo kadhaa ndani ya miaka mitatu au minne, baada ya Pauni Milioni 70 kulipwa taslimu. 
  World stage: Real Madrid seem to be setting up a stage at the Bernabeu, with Gareth Bale close to joining
  Jukwa kali: Real Madrid inaonekana kuandaa jukwaa maalum kwa ajili ya kumtambulisha Bale Uwanja wa Bernabeu

  Real Madrid inacheza na Granada Jumatatu usiku katika La Liga na kama kutambulishwa kwa Bale itakuwa Jumanne.
  Bale, ambaye alijiunga na Spurs kwa dau la Pauni Milioni 10 kutoka Southampton mwaka 2007, alishinda tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Chama cha Wachezaji wa Kulipwa na Waandishi wa Soka msimu uliopita, ameifungia mabao 26 timu ya White Hart Lane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: BALE ATUA HISPANIA KUKAMILISHA USAJILI WAKE WA REKODI YA DUNIA REAL MADRID Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top