• HABARI MPYA

  Ijumaa, Agosti 30, 2013

  MWANTIKA WA AZAM ACHUKUA NAFASI YA YONDAN TAIFA STARS

  Na Boniface Wambura, IMEWEKWA AGOSTI 30, 2013 SAA 10:25 JIONI 
  KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Kim Poulsen amemuongeza kwenye kikosi chake beki David Mwantika wa Azam FC kwa ajili ya mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
  David Mwantika amechukua nafasi ya Yondan Stars

  Mwantika ameitwa kwenye kikosi hicho kuziba nafasi ya beki Kevin Yondani ambaye ni majeruhi. Wachezaji ambao ni majeruhi na Kim amewaondoa kwenye kikosi hicho ili waweze kushughulikia matibabu yao ni Athuman Idd, Shomari Kapombe na John Bocco.
  Kevin Yondan ameenguliwa Stars sababu ya majeruhi 

  Taifa Stars imeingia kambini na kuanza mazoezi leo jioni kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume. Timu hiyo inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager pia itakuwa ikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Taifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments
  Item Reviewed: MWANTIKA WA AZAM ACHUKUA NAFASI YA YONDAN TAIFA STARS Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top