• HABARI MPYA

    Monday, August 19, 2013

    KAMA KAWAIDA, MOURINHO AANZA DOMO ENGLAND, ASEMA "NIMEKUJA KUWASHIKA"

    IMEWEKWA AGTOSTI 19, 2013 SAA 1:34 USIKU
    KOCHA Jose Mourinho ametoa onyo kwa wapinzani wake Jumapili baada ya kurejea rasmi katika Ligi Kuu ya England.
    Ametoa ujumbe wa moja kwa moja kwa wapinzani wa Chelsea katika mbio za ubingwa, kufuatia ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Hull City, kisha akwaonya Manchester United kwamba hajaachana na mpango wake wa kutaka kumsajili Wayne Rooney.
    Kocha huyo wa Stamford Bridge amethibitisha atapigania saini ya mshambuliji huyo wa England hadi pazia la usajili wa majira haya ya joto litakapofungwa Septemba 2 na BIN ZUBEIRY inafahamu iwapo hatofanikiwa atajaribu tena katika dirisha la Januari.
    VIDEO Kaangalie Jose: Tutampigania Rooney hadi siku ya mwisho
    Boost: Jose Mourinho said that having Roman Abramovich in the dressing-room is a huge help
    Mkali: Jose Mourinho amesema kuwa na Roman Abramovich chumba cha kubadilishia nguo ni msaada mkubwa

    Mourinho hakutaka kutaja jina la Rooney, lakini alisema: "Unafahamu wachezaji gani — tunaweza kupambana na mazingira wakati wote katika njia ya uadilifu.’
    Klabu hiyo itatuma ofa nyingine, ambayo inaaminika itakuwa Pauni Milioni 40, kwa ajili ya mshambuliaji huyo wa United wiki hii. 
    Chelsea ilimtaka Robert Lewandowski na kwa bahati mbaya kwao, akachafua kubaki Borussia Dortmund kwa mwaka mwingine mmoja kabla ya kujiunga na Bayern Munich msimu ujao. 
    Chelsea itakuwa na mazungumzo na wawakilishi wa Samuel Eto’o Jumanne wakiwa na nia ya kumsajili kwa muda mfupi. 
    Jose: Tutampigania Rooney hadi siku ya mwisho
    Unsettled: Wayne Rooney watched the first half of United's match against Swansea from the bench
    Hajatulia: Wayne Rooney aliangalia kipindi cha kwanza United ikicheza na Swansea akiwa benchi Jumamosi
    All smiles: Abramovich looked happy with the way in which Chelsea kicked off their campaign
    Tabasamu: Abramovich akionekana mwenye furaha namna Chelsea ilivyoanza msimu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: KAMA KAWAIDA, MOURINHO AANZA DOMO ENGLAND, ASEMA "NIMEKUJA KUWASHIKA" Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top