• HABARI MPYA

    Saturday, August 17, 2013

    WENGER AANZA VIBAYA LIGI KUU ENGLAND, AFUMULIWA 3-1 NA VILLA NA MAJERUHI WAONGEZEKA

    IMEWEKWA AGOSTI 17, 2013 SAA 3:21 USIKU
    KOCHA Arsene Wenger ameanza vibaya Ligi Kuu ya England baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Aston Villa Uwanja wa Emirates leo.
    Kocha huyo Mfaransa amesaini mchezaji mmoja tu ambaye pia ni majeruhi baada ya kutemwa wachezaji 17.
    Wachezaji wawili wa Arsenal, Keiron Gibbs na Alex Oxlade-Chamberlain walilazimika kutoka nje kipindi cha kwanza baada ya kuumia na Christian Benteke alikuwa kinara wa ushindi wa Villa.
    Benteke alifunga mabao mawili katika dakika za 21na 60 wakati bao lingine lilifungwa na Luna dakika ya 84, wakati Arsenal ilitangulia kupata bao dakika ya tano kupitia kwa Olivier Girous.
    Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Sagna/Podolski dk90, Koscielny, Mertesacker, Gibbs/Jenkinson dk5, Wilshere, Ramsey, Rosicky, Walcott, Chamberlain/Cazorla dk5 na Giroud
    Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker/Clark dk7, Luna, El Hamadi, Westwood, Delph, Agbonlahor, Weimann/Bacuna dk88 na Benteke,
    VIDEO Kaangalia chini Paul Lambert: Agbonlahor na Benteke
    Neat finish: Arsenal's Olivier Giroud, left, opens the scoring
    Mshambuliaji wa Arsenal, Olivier Giroud akifunga bao la kuongoza
    Arsenal v Aston Villa possession stats - taken from MailOnline's new Match Zone
    Takwimu za mechi ya Arsenal na Aston Villa
    Sharp shooter: Giroud celebrates his goal
    Giroud akishangilia
    Saved: Arsenal's Wojciech Szczesny keeps out Benteke's penalty...
    Ameokoa: Kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny akipangua mkwaju wa penalti wa Benteke...
    benteke
    ...lakini Benteke akafunga baada ya kuuwahi mpira uliorudi

    Bloodied: Arsenal's Kieran Gibbs lies on the floor with a cut head after a clash of heads with Villa's Andreas Weimann
    Damu: Mchezaji wa Arsenal, Kieran Gibbs akiigulia maumivu chini baada ya kugongana na Andreas Weimann wa Villa
    Gibbs is escorted off the pitch with a head injury
    Gibbs akitolewa baada ya kuumia kichwa
    Heads up: Villa's Ron Vlaar, second right, clears the ball
    Mchezaji wa Villa, Ron Vlaar, wa pili kulia akiokoa
    Committed: Arsenal's Tomas Rosicky, below, tackles Villa's Karim El Ahmadi
    Mchezaji wa Arsenal, Tomas Rosicky, chini akipambana na Karim El Ahmadi wa Villa
    Controversy: Santi Cazorla, Per Mertesacker and Wojciech Szczesny cannot believe that referee Anthony Taylor has awarded a second penalty
    Utata: Santi Cazorla, Per Mertesacker na Wojciech Szczesny wakiwa hawaamini refa Anthony Taylor amewapa Villa penalti ya pili
    Splash the cash: An Arsenal fan sends a clear message to Wenger
    Shabiki wa Arsenal akipeleka wa wazi kwa Wenger kumtaka asajili
    Arsenal manager Arsene Wenger looks dejected on the touchline
    Mwanzo mbaya: Wenger akisikitika baada ya kipigo

    Katika mchezo mwingine, bao pekee la Daniel Sturridge dakika ya 37, lilitosha kuipa Liverpool ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Stoke City.
    Kikosi cha Liverpool kilikuwa: Mignolet, Johnson, Toure, Agger, Enrique, Lucas, Henderson, Gerrard, Coutinho, Sturridge, Aspas/Sterling dk71.
    Stoke: Begovic, Cameron, Huth, Shawcross, Pieters, N'Zonzi, Whelan/Adam dk62, Wilson, Etherington/Pennant dk62, Walters na Crouch/Jones dk81.
    New Suarez? Sturridge celebrates the opening goal after his fierce drive
    Suarez mpya? Sturridge akifunga 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: WENGER AANZA VIBAYA LIGI KUU ENGLAND, AFUMULIWA 3-1 NA VILLA NA MAJERUHI WAONGEZEKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top