• HABARI MPYA

    Sunday, August 04, 2013

    DROGBA AWATUNGUA MARA MBILI ARSENAL NA KUIPA GALATASARAY KOMBE LA EMIRATES LEO, WENGER HOI HADI UTAMUONEA HURUMA

    IMEWEKWA AGOSTI 4, 2013 SAA 4:35 USIKU
    MSHAMBULIAJI Didier Drogba ameendelea kuwa mwiba kwa Arsenal akikumbushia enzi zake alipokuwa na jezi ya Chelsea, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 35 leo kufunga mabao mawili na kuiwezesha klabu yake, Galatasaray kutwaa Kombe la Emirates.
    Kweli, ni mashindano ya kirafiki na hayana maana yoyote katika msimu, lakini lilikuwa kama pigo lingine kwa kikosi cha Arsene Wenger.
    Mfaransa huyo aliwaka ile mbaya kana kwamba mashindano hayo yana maana yoyote. Alimfokea refa wa akiba, Andre Marriner baada ya refa Jon Moss kuwazawadia penalti wapinzani dakika 12 kabla ya filimbi ya mwisho kutokana na Ignasi’s Miquel kumsukuma mshambuliaji huyo wa Ivory Coast.
    Drogba alikwenda mwenyewe kupiga penalti hiyo na kumpeleka upande tofauti kipa Wojciech Szczesny na mpira alipoupiga. 
    Drogba akafunga tena zikiwa zimesalia dakika nne, baada ya kupokea pasi ya Wesley Sneijder na kumuacha Per Mertesacker, kabla ya kumtungua tena Szczesny.
    Arsenal ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao katika mchezo huo dakika ya 38, mfungaji Theo Walcott. 
    Katika mchezo huo, kikosi cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Jenkinson, Sagna, Mertesacker, Gibbs/Miquel dk69, Arteta, Ramsey, Oxlade-Chamberlain, Cazorla/Zelalem dk61, Walcott na Sanogo/Giroud dk61.
    Galatasaray Muslera; Semih, Riera, Chedjou, Eboue, Melo/Sarioglu dk66, Engin Baytar/Gulselam dk32,Altintop/Colak, dk45, Amrabat, Elmander/Drogba dk45, Umut Bulut/Sneijder dk45.
    On target: Drogba scored a late double to clinch the Emirates Cup
    Amefunga: Drogba amefunga mabao dakika za lala salama Kombe la Emirates leo
    Spot on: Drogba sends Wojciech Szczesny the wrong way
    Kitu nyavuni: Drogba akimuuza Wojciech Szczesny
    Remember me? Drogba celebrates after the final whistle
    Mnanikumbuka? Drogba akishangilia baada ya kufunga bao la pili
    Opener: Walcott watched his cross-come-shot give Arsenal the lead
    La kwanza: Walcott akishuhudia krosi yake ikiipa Arsenal bao la kuongoza
    Smiles all round: Walcott celebrates with his Arsenal teammates
    Walcott akishangilia na wachezaji wenzake wa Arsenal
    Return home: Emamanuel Eboue (right) captained Galatasaray on his return to former club Arsenal
    Amerudi nyumbani: Emamanuel Eboue (kulia) alikuwa Nahodha wa Galatasaray ilipomenyana na timu yake ya zamani leo, Arsenal
    New man: Yaya Sanogo made a promising start in his first Emirates appearance
    Mtu mpya: Yaya Sanogo ameng'ara katika michuano yake ya kwanza ya Kombe la Emirates
    No holding back: Johan Elmander of Galatasaray battles with Kieran Gibbs of Arsenal
    Johan Elmander wa Galatasaray akipambana na Kieran Gibbs wa Arsenal
    Disappointment: Arsenal manager Arsene Wenger looks on during his side's defeat
    Kadata na kichapo: Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alivyokuwa baada ya kipigo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments
    Item Reviewed: DROGBA AWATUNGUA MARA MBILI ARSENAL NA KUIPA GALATASARAY KOMBE LA EMIRATES LEO, WENGER HOI HADI UTAMUONEA HURUMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top