• HABARI MPYA

    Tuesday, June 06, 2023

    AZAM FC YAIKANDAMIZA COASTAL UNION 2-0 PALE PALE MKWAKWANI


    TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
    Mabao ya Azam FC leo yamefungwa na washambuliaji wake tegemeo, Idris Mbombo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) dakika ya 58 na Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 90.
    Azam FC inafikisha pointi 56, ingawa inabaki nafasi ya tatu, wakati hali ni mbaya kwa Coastal Union inayobaki na pointi zake 33 nafasi ya 10 baada ya wote kucheza mechi 29.
    Mechi nyingine za Ligi Kuu, Yanga  imetoka nyuma kwa mabao matatu kupata sare ya 3-3 na wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
    Mabao ya Yanga yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison mawili dakika za 33 na 90 na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 68, baada Mbeya City kutangulia na mabao ya George Sangija dakika ya tatu, Richardson Ng’ondya dakika ya 43 na 52.
    Yanga inafikisha pointi 75 kileleni, wakati Mbeya City inafikisha pointi 31 nafasi ya 12.
    Nayo Mtibwa Sugar imeichapa Kagera Sugar 3-0 mabao ya Mayanga dakika ya 33, Omary dakika ya 45 na Mfuko aliyejifunga dakika ya 66 Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
    Mechi nyingine Singida Big Stars imeshinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa LITI mjini Singida, Tanzania Prisons imeichapa KMC 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa na Ihefu imeichapa Geita Gold 3-1 Uwanja wa Highland Estate Mbarali mkoani Mbeya.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: AZAM FC YAIKANDAMIZA COASTAL UNION 2-0 PALE PALE MKWAKWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top