• HABARI MPYA

  Tuesday, June 06, 2023

  MORRISON APIGA MBILI YANGA YADROO 3-3 NA MBEYA CITY


  MABINGWA, Yanga SC wametoka nyuma kwa mabao matatu kupata sare ya kufungana mabao 3-3 na wenyeji, Mbeya City katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Yanga yamefungwa na winga Mghana, Bernard Morrison mawili dakika za 33 na 90 na Salum Abubakar ‘Sure Boy’ dakika ya 68, baada Mbeya City kutangulia na mabao ya George Sangija dakika ya tatu, Richardson Ng’ondya dakika ya 43 na 52.
  Yanga inafikisha pointi 75 kileleni, wakati Mbeya City inafikisha pointi 31 nafasi ya 12.
  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo, mabao ya Idris Mbombo dakika ya 58 na Prince Dube dakika ya 90 yameipa Azam FC ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Coastal Union Uwanja wa Mkwakwani Jijini Tanga.
  Nayo Mtibwa Sugar imeichapa Kagera Sugar 3-0 mabao ya Mayanga dakika ya 33, Omary dakika ya 45 na Mfuko aliyejifunga dakika ya 66 Uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
  Mechi nyingine Singida Big Stars imeshinda 2-1 dhidi ya Ruvu Shooting Uwanja wa LITI mjini Singida, Tanzania Prisons imeichapa KMC 1-0 Uwanja wa Nelson Mandela mjini Sumbawanga mkoani Rukwa na Ihefu imeichapa Geita Gold 3-1 Uwanja wa Highland Estate Mbarali mkoani Mbeya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MORRISON APIGA MBILI YANGA YADROO 3-3 NA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top