• HABARI MPYA

    Sunday, March 12, 2023

    DODOMA JIJI YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 JAMHURI

    WENYEJI, Dodoma Jiji FC wameibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.
    Mabao ya Dodoma Jiji yamefungwa na Seif Karihe dakika ya 49 na Collins Opare dakika ya 54, wakati la Polisi Tanzania limefungwa na Ibrahim Ahmada Hilika dakika ya 89.
    Kwa ushindi huo, Dodoma Jiji FC inafikisha pointi 27 na kusogea nafasi ya 11, wakati Polisi Tanzania inabaki na pointi zake 19 ikiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.
      
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: DODOMA JIJI YAICHAPA POLISI TANZANIA 2-1 JAMHURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top