• HABARI MPYA

  Jumamosi, Agosti 01, 2020

  ARSENAL WATWAA KOMBE LA FA BAADA YA KUICHAPA CHELSEA 2-1

  Nahodha Pierre-Emerick Aubameyang akiwa ameinua Kombe la FA baada ya kuiongoza Arsenal kubeba hilo kwa ushindi wa 2-1 dhidi ya Chelsea Uwanja wa Wembley Jijini London usiku wa leo. Chelsea walitangulia kwa bao Christian Pulisic dakika ya tano kabla ya Aubameyang kusawazisha kwa penalti dakika ya 28 na kufunga la ushindi dakika ya 67 kuipa The Gunners taji la 14 la FA akiwa amevaa jezi namba 14 mgongoni. Chelsea ilimaliza pungufu baada ya Mateo Kovacic kutolewa kwa kadi nyekundu na refa Anthony Taylor kufuatia kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dakika ya 72 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ARSENAL WATWAA KOMBE LA FA BAADA YA KUICHAPA CHELSEA 2-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top