• HABARI MPYA

  Jumatatu, Januari 06, 2020

  NDUNDA AIPELEKA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI BAADA YA KUOKOA PENALTI MBILI LEO PEMBA

  Kipa Said Mohammed 'Ndunda' akipongezwa na mlinda mlango mwenzake, Abutwalib Msheri baada ya kuokoa penalti mbili na kuiwezesha Mtibwa Sugar kutinga Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa penalti 4-2 dhidi ya Chipukizi FC baada ya sare ya 1-1 leo Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba kwenye mchezo wa Kund B. Chipukizi ilitangulia kwa bao la Suleiman Nassor dakika ya tano, kala ya Haroun Chanongo kuisawazishia Mtibwa Sugar dakika ya 63.
  Nduda aliokoa penalti za Jumaa Kassim na Abdallah Mohamed, wakati mikwaju ya Salim Abui na Abdalla Khalisan ilimpita huku penalti za Mtibwa Sugar zilifungwa na Omar Sultan, Abdulhalim Humud, Riffat Khamis na Dickson Job.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NDUNDA AIPELEKA MTIBWA SUGAR NUSU FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI BAADA YA KUOKOA PENALTI MBILI LEO PEMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top