• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 26, 2019

  MECHI YA YANGA NA TANZANIA PRISONS YAHAMISHIWA UWANJA WA SAMORA MJINI IRINGA KESHO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baina ya wenyeji, Tanzania Prisons na Yanga SC ya Dar es Salaam uliokuwa ufanyike Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya sasa utafanyika kesho Uwanja wa Samora mjini Iringa.
  Hiyo ni baada ya Uwanja wa Sokoine kuharibika katika eneo la kuchezea kufuatia tamasha la muziki lililofanyika usiku wa kuamkia leo, hivyo Bodi ya Ligi kuamua kuuzuia uwanja huo kutumika kwa mechi zote za Ligi zinazotambuliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). 
  Yanga SC ipo mjini Mbeya tangu Jumapili na Jumanne ilicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wengine na kutoa sare ya 0-0.

  Kikosi hicho chini ya kocha wake Mkuu, Charles Boniface Mkwasa kitaondoka leo usiku kwenda Iringa, umbali wa kilomita zisizopungua 278 tayari kwa mchezo wa kesho jioni.
  Ligi Kuu ya Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja tu, Coastal Union wakiikaribisha Azam FC Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga na kesho kutwa, mabingwa watetezi, Simba SC watamenyana na KMC Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MECHI YA YANGA NA TANZANIA PRISONS YAHAMISHIWA UWANJA WA SAMORA MJINI IRINGA KESHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top