• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 24, 2019

  YANGA SC YATOA SARE YA PILI MFULULIZO LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MBEYA CITY LEO SOKOINE

  Na Mwandishi Wetu, MBEYA
  YANGA SC imetoa sare ya pili mfululizo leo katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya kumaliza mchezo bila kufungana na wenyeji, Mbeya City Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.
  Sare hiyo inayoifuatia ile ya 1-1 na KMC Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam Desemba 2, inaifanya Yanga ifikishe pointi 18 katika mchezo wa tisa, sasa ikizidiwa pointi saba na vinara, Simba SC ambao pia ni mabingwa watetezi, ingawa wamecheza mechi moja zaidi.
  Katika mchezo wa leo, Yanga ilionekana kabisa kuathiriwa na kuwakosa wachezaji wake muhimu wa kikosi cha kwanza waliokuwa vikosi vya Tanzania Bara na Zanzibar nchini Uganda kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge.

  Hao ni beki Ali Ali, viungo Abdulaziz Makame, Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Mohammed Issa ‘Banka’ waliokuwa na timu ya Zanzibar na kipa Metacha Mnata na beki Kelvin Yondan wa Bara.
  Yanga itabaki mjini Mbeya kwa mchezo mwingine wa Ligi Kuu dhidi ya wenyeji wengine, Tanzania Prisons Ijumaa hapo hapo Uwanja wa Sokoine. 
  Kikosi cha Mbeya City kilikuwa; Haroun Mandanda, Kenny Kunambi, Hassan Mwasapili, Samson Madeleke, Baraka Johnson, Edgar Mbembela, Suleiman Mangoma/Notikelly Masasi dk85, George Chota, Iddi Gamba/Kelvin John dk79, Peter Mapunda na Suleiman Ibrahim/Majaliwa Shaaban dk67.
  Yanga SC; Farouk Shikharo, Mustapha Suleiman, Jaffar Mohammed, Lamine Moro, Ally Mtoni ‘Sonso’, Said Juma ‘Makapu’/Mrisho Ngassa dk61, Deus Kaseke, Papy Kabamba Tshishimbi, David Molinga, Raphael Daudi na Patrick Sibomana.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YATOA SARE YA PILI MFULULIZO LIGI KUU, YATOKA 0-0 NA MBEYA CITY LEO SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top