• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 26, 2019

  MAREFA WA BURUNDI KUICHEZESHA TANZANIA DHIDI YA UGANDA KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U20

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MCHEZO wa kufuzu Kombe la Dunia Uganda dhidi ya Tanzania Wanawake U20 utachezeshwa na Waamuzi kutoka Burundi.
  Mchezo huo utakaochezwa kati ya Disemba 31, 2019,Januari 1,2,2020 Uganda Mwamuzi wa katikati Darlene Nduwayo ambaye atasaidiwa na Fides Bangurambona na Alida Iradukunda,Mwamuzi wa akiba Aline Umutoni wakati Kamishna wa mchezo Tesfaneshi Woreta anatokea Ethiopia.
  Mchezo wa marudiano wenyewe utachezwa kati Tanzania ya Januari 17,18 na 19,2020 na utachezeshwa na Waamuzi kutoka Kenya.
  Mwamuzi wa katikati Agnet Napangor atakayesaidiwa na Mary Njoroge na Carolyne Njoroge,Mwamuzi wa akiba Carolyne Wanjala na Kamishna wa mchezo Tharcile Uwamahoro kutoka Rwanda
  Waamuzi kutoka Kenya watachezesha mchezo wa kufuzu Kombe la Dunia Tanzania dhidi ya Burundi Wasichana U17.
  Mwamuzi wa Katikati Agnet Napangor atasaidiwa na Jane Cherono na Carolyne Chemtai na Mwamuzi wa akiba atakua Carolyne Wanjala.
  Kamishna wa mchezo Vololona Rejeriarison anatokea Madagascar na Mtathmini Waamuzi Constance Wejeli Adipo kutoka Uganda.
  Mchezo huo utachezwa kati ya Januari 10,11 na 12,2020.
  Nao Waamuzi kutoka Eritrea watachezesha mchezo wa marudiano utakaochezwa kati ya Januari 17,18 na 19,2020 Burundi.
  Mwamuzi wa katikati Yodit Hagos atasaidiwa na Elisa Ghebrab Yohanes na Tsega Hassen,na Mwamuzi wa akiba Lidya Tafesse.
  Kamishna wa mchezo Leocadie Ngwema anatokea Gabon na Mtathmini Waamuzi Nima Boulaleh anatoka Djibouti. Mchezo utachezwa kati ya Januari 17,18 na 19,2020 Burundi
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WA BURUNDI KUICHEZESHA TANZANIA DHIDI YA UGANDA KUFUZU KOMBE LA DUNIA WANAWAKE U20 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top