• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 14, 2019

  STARS YATINGA NUSU FAINALI CECAFA CHALLENGE BAADA YA SARE YA 0-0 NA SUDAN LEO KAMPALA

  Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
  TANZANIA Bara imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya michuano ya Kombe la Maitafa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya sare ya 0-0 na Sudan katika mchezo wa kundi B jioni ya leo Uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda.
  Kwa matokeo hayo, Kilimanjaro Stars inayofundishwa na kocha Juma Mgunda anayesaidiwa na Zubery Katwila inamaliza na pointi nne baada ya kushinda mechi moja dhidi ya Zanzibar 1-0 na kufungwa 1-0 na Kenya katika mchezo wa kwanza.
  Kilimanjaro Stars yenyewe itamenyana na ama Eritrea, Somalia au Djibouti zinazowania kumaliza nafasi ya pili nyuma ya wenyeji, Uganda. 
  Uganda tayari ina pointi tisa baada ya kushinda mechi zake tatu, ikifuatwa na Eritrea pointi sita, Somalia pointi nne sawa na Djibouti, wakati Burundi inashika mkia baada ya kufungwa mechi zote nne.

  Baada ya kuichapa Zanzibar 1-0, bao pekee la Oscar Wamalwa dakika ya 48 Harambee Stars inafuzu Nusu Fainali kama kinara wa Kundi B kwa pointi zake tisa, huku Sudan iliyomaliza ya tatu kwa pointi zake mbili na Zanzibar iliyoshika mkia kwa ponti yake moja zikirejea nyumbani.
  Kikosi cha Tanzania Bara kilikuwa; Aishi Manula, Mwaita Gereza/Nickson Kibabage dk91+3, Gardiel Michael, Bakari Mwamnyeto, Kelvin Yondani, Jonas Mkunde, Hassan Dilunga, Muzamil Yassin, Miraji Athumani ‘Madenge’/ Cleophace Mkandala dk21, Ditram Nchimbi na Eliuter Mpepo/Paul Nonga dk77.
  Sudan; Mohamed Abudalla, Ahmed Ibrahim Ahmed/ Shakhaldeen Mohamed dk78, Rami Abdallah Krdgil Ganddil, Montasir Osman Yahia, Amr Mubarak Abdalla, Ammar Mohamed, Magdi Mohamed Abdellatif/ Mohamed Humidan dk51, Ammar Yaser/ Munir Yassin dk62, Moaiad Abdeen Maki, Mohamed Abbas Namir na Bakhit Khamis.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS YATINGA NUSU FAINALI CECAFA CHALLENGE BAADA YA SARE YA 0-0 NA SUDAN LEO KAMPALA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top