• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 30, 2019

  YANGA SC YAJISOGEZA NYUMA KABISA YA SIMBA SC LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imepanda hadi nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Biashara United ya Musoma mkoani Mara jioni ya leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Shukrani kwa bao pekee la mshambuliaji mpya, Tariq Seif Kiakala dakika ya 84 akimalizia pasi ya Nahodha na kungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi kuiadhibu timu yake ya zamani.
  Na kwa ushindi huo, Yanga SC inayofundishwa na gwiji wake, Charles Boniface Mkwasa inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 11 na kupanda hadi nafasi ya pili, ikiizidi wastani wa mabao tu Kagera Sugar na sasa inazidiwa pointi saba na mabingwa watetezi, Simba SC.


  Mechi nyingine za Ligi Kuu leo; Coastal Union imeshinda 2-0 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, Lipuli FC imeichapa Mbao FC 3-0 Uwanja wa Samora Iringa, Ruvu Shooting imeichapa Kagera Sugar 2-1 na Alliance FC wameshinda 1-0 dhidi ya wenyeji, Mtibwa Sugar Uwanja wa CCM Gairo.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Metacha Mnata, Mustafa Suleiman, Adeyoum Ahmed, Lamine Moro, Ally Mtoni ‘Sonso’, Abdullaziz Makame, Deus Kaseke, Feisal Salum/ Mapinduzi Balama dk46, David Molinga/ Tariq Seif dk46, Mrisho Ngassa/Papy Kabamba Tshishimbi dk69 na Patrick Sibomana.
  Biashara United; Danel Mgore, Wilfred Kauruma, Novatus Dismass, Derick Mussa, Justine Bilary/Mustafa Khamis dk79, James Mwasote, Abdulmajid Mangaro, Bright Obina, Mpapi Nassib, Ramadhani Chombo ‘Redondo’ na Joseph Kimwaga/Ally Kombo dk79.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAJISOGEZA NYUMA KABISA YA SIMBA SC LIGI KUU BAADA YA KUICHAPA BIASHARA UNITED 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top