• HABARI MPYA

  Friday, December 13, 2019

  YANGA SC YATOKA NYUMA NA KUSHINDA 2-1 DHIDI YA MWAMGONGO FC LEO MJINI KIGOMA

  Na Mwandishi Wetu, KIGOMA
  YANGA SC imepata ushindi wa 2-1 dhidi ya Mwamgongo FC katika mchezo wa kirafiki jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
  Hadi mapumziko, tayari Yanga SC walikuwa mbele kwa 2-1, mabao yake yakifungwa na Mapinduzi Balama dakika ya 19 na Adam Stanley dakika ya 34, kufuatia wenyeji, Mwamgongo kutanguliwa kwa bao la Abdulrazak Boban dakika ya 14.
  Yanga SC watateremka tena dimbani Jumapili katika mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya wapinzani wao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Mbao FC.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Ramadhani Kabwili, Vincent Paschal, Muharami Issa ‘Marcelo’, Cleophace Sospeter, Mustafa Suleiman, Said Juma ‘Makapu’, Mussa Said, Mapinduzi Balama, Adam Stanley, Raphael Daudi na Gustapha Simon. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATOKA NYUMA NA KUSHINDA 2-1 DHIDI YA MWAMGONGO FC LEO MJINI KIGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top