• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 26, 2019

  KWA MADUDU HAYA YA MAREFA WETU, TUSUBIRI HIYO JANUARI 4

  Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
  Hakika ilikuwa ni siku ambayo mvua iliishibisha vilivyo ardhi kwa kuipa maji mpaka mengine yakawa hayana pakwenda na kuonekana kutuama.
  Nikiwa na vazi langu lililo lowanishwa na mvua hiyo vilivyo nilikimbiq hadi kwenye moja ya kibanda umiza kilichokuwa karibu na eneo nililokuwa nimejificha mvua.
  Nilipoingia nilichukua nafasi yangu ya kukaa na kuyaweka macho yangu kwenye runinga ili kushuhudia soka la kulevya la nchi yangu ninayo ipenda.
  Mchezo uliokuwa unaendelea hapo ulikuwa ni mchezo wa ligi kuu. mechi kati ya Mabingwa wa kihistoria wa ligi hiyo na watoto wa walima mpunga wa mbeya.

  Nikiwa hapo mzee mmoja akatoa kauli moja ambayo ilianza nifanye kufikiria hili"ili tatizo la waamuzi hapa nchini ni sawa na ugonjwa wa pumu tu,unarithiwa tu"
  Mara ya kwanza niliona huenda babu huyu ameanza kulevywa na kahawa alizotoka kunywa kabla ya kuingia kwenye kibanda hicho lakini halmashauri ya ubongo wangu ikawa inanipa ishara kuwa Ndani ya Masijara ya kichwa changu kuna faili ambalo limeingia mda sio mrefu natakiw Kulifungua.ili kupata kujua maana ya kauli ya mzee huyo.
  Haraka nikaingia na kulifungua faili hilo kujionea kilicho andikwa.
  Ndani ya faili hilo nilikutana na sauti yangu niliyowaho kujirekodi miaka kadhaa iliyopita wakati naanza kazi ya uchambuzi wa soka kwenye moja ya kituo cha redio hap Nchini.
  Nakumbuka niliwahi kusema kuwa shoda kubwa ya waamuzi wa hapa nchini ni namna wanavyo andaliwa kuanzia huko wanapotokea  hadi hapa  wanapofikia.
  Waamuzi wetu hiki wanacho kifanya kunako ligi kuu ni kama tabia yao ambayo ilikuwa kama maisha yao halisi walipokuwa wanafanya kazi kuanzia ligi  daraja la kwanza la pili na kushuka chini.
  Matukio yanayo onekana ligi kuu ni sehemu ndogo kati ya mengi yanayofanywa  kwenye hizi ligi za chini.
  Ikiwa hawa ambao wapo huku ligo daraja la kwanza.ndo tunategemea kuwapandisha waje kuchezesha ligi kuu, alafu  hawa ndo wanaongoza kwa kuwa na matatizo mengiii ambayo mengine hayasemeki , je ni kweli ugonjwa huu wa pumu utaacha kuathiri vizazi na  vizazi ? 
  Kama ni kweli tuna ndoto za kuja kupata waamuzi bora na wasio na mashaka.kwanza tuanze kuwaangalia hawa walio chini ambao kesho ndo tunategemea kuwapandisha juu.kwa sababu hawa wa juu tayari ugonjwa umesha waathiri na hawawezi kupona kamwe.maana pumu ikikomaaa mtu haponi anapata afueni tu😁.
  Tatizo la waamuzi ni la dunia nzima lakini ya kwetu yana onekana kuwa yamezidia sana.
  Kwa mujibu wa faili langu kuna ukurasa unasema kuwa usipoziba ufa utajenga ukuta.
  Kuna kipengele cha sheria kumi na saba za mpira wa miguu lazima kiheshimiwe kinachosema kuwa 'Referee decision is an apinion'
  Kuna mda maamuzi yake yaheshimiwe japo sio kila akiamuacho kinaweza kuwa sahihi kuna mda kama binaadamu huwa anakosea na kuna mda Pumu yake humjia baada ya kuona meseji ya muamala hata akazidiwa na akafanya kinyume.
  Kwa leo ubongo wangu una nambia faili limefika mwisho japo kina kumbu kumbu iliyobakia lakini ubongo wangu unasema niiache maana akili hii inasema kuwa waratibu wa ugonjwa huu wapo kwenye shrikisho letu la soka.
  Jamani kwaherini maana kila nikifikiria ubongo wangu unazidi kunipa kumbukumbu zilizojificha.
  Mimi acha niisubiri tarehe nne huenda nikamuona mgonjwa mwengine wa pumu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KWA MADUDU HAYA YA MAREFA WETU, TUSUBIRI HIYO JANUARI 4 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top