• HABARI MPYA

  Jumapili, Desemba 15, 2019

  SAMATTA AINGIA BADO DAKIKA 13 KRC GENK YAICHAPA WAASLAND-BEVEREN 4-1 LIGI YA UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, GENK
  MSHAMBULAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta usiku wa jana alitokea benchi zikiwa zimesalia dakika 13 na ushei na kuisadia timu yake, KRC Genk kupata ushindi wa 4-1 dhidi ya Waasland-Beveren katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk.
  Samatta alitokea benchi zikiwa zimesalia dakika 13 na ushei kwenda kuchukua nafasi ya mshambuliaji mwenzake, Mbelgiji Theo Bongonda Mbul'Ofeko Batombo wakati huo tayari KRC Genk inaongoza 4-0.
  Mabao ya Genk yalifungwa na Bongonda dakika ya 10, Mnigeria Ebere Paul Onuachu dakika ya 26, Mcolombia Jhon Janer Lucumí dakika ya 35 na Mnorway Sander Berge dakika ya 70, wakati la Waasland-Beveren lilifungwa na Mserbia, Aleksandar Vukotic dakika ya 88.
  Kwa ushindi huo, mabingwa hao watetezi, Genk wanafikisha pointi 28 katika mechi ya 19 na kupanda kwa nafasi moja hadi ya saba, wakiwa wanazdiwa pointi 14 na vinara, Club Brugge ambao hata hivyo wana mechi mbili mkononi.
  Jana Samatta amecheza mechi ya 181 katika katika mashindano yote akiwa amefunga mabao 71 tangu ajiunge na KRC Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
  Katika ligi ya Ubelgiji pekee amecheza mechi 140 akiwa amefunga mabao 54, kwenye Kombe la Ubelgiji amecheza mechi 10, amefunga mabao mawili, katika Super Cup mechi moja na Ligi ya Mabingwa Ulaya mechi sita, mabao matatu.
  Kikosi cha KRC Genk kilikuwa; Vandevoordt, Maehle, Dewaest, Lucumi, Neto, Berge, Hrosovsky, Ito, Bongonda/Bongonda dk76, Paintsil/Hagi dk68 na Onuachu/Wouters dk83.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SAMATTA AINGIA BADO DAKIKA 13 KRC GENK YAICHAPA WAASLAND-BEVEREN 4-1 LIGI YA UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top