• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 18, 2019

  HIZI NI SALAMU ZANGU KWA DITRAM NCHIMBI NA SAFARI YAKE YANGA SC

  Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
  Safari ya kutoka jijini mwanza hadi kufika jijini Dar es salaam ilitamatika kwa muda wa takribani masaa 21.
  Majira ya saa Sita Usiku ndio usafiri wa gari ya moja ya kampuni maaruufu hapa Nchini iliweza kukanyaga katika Ardhi ya jiji la Dae es salaam.
  Nikiwa nimesombwa na uchovu wa safari hiyo ndefu.huku nikiwa na mizigo lukuki.nilitembea mpaka katika moja ya vijiwe vya kupaki Usafiri wa Boda boda ili kuchukua Usafiri.
  Wakati nimesimama hapo nilimshuhudia kijana mmoja wa makamo akiwa amevalia Jezi ya timu maarufu saana Afrika ya mashariki na Kati YOUNG AFRICANS.
  Akiwa amesimama mbele ya Madereva Boda boda wenzake nilimsikia akitamba kwa kusema.
  "tumelea kifaa kipya,watani zetu mjiandae na mauaji iyo siku ya Tarehe Nne .anaitwa Ditram Nchimbi"
  Kauli yake ikasisimua ubongo wangu.ikaamsha hali ya kufikiri kwenye Kichwa changu na kunifanya nianze kumfikiria Mchezaji uyu na jukumu zito analokwenda kukutana nalo.
  Haraka nikafungua begi langu kisha nikatoa kalamu na karatasi kisha nikaanza kuandika salamu zangu kuelekea kwake Ditram Nchimbi.
  Kwako Nchimbi,
  Hakika kwanza nikupongeze kwa nafasi hii adhimu uliyoipata maana si wote wanaobahatika kucheza kwenye Klabu hiyo ya Yanga.
  Tambua umebeba matuamini ya wana Yanga walio wengi wanao lifananisha jina lako na Majina makubwa yaliyowahi kupita klabuni hapo.
  Tambua kupitia miguu yako wana Yanga wana matumani makubwa ya kufunua vinywa vyao kwa furaha ya miguu hiyo kutikisa nyavu za timu pinzani.
  Tambua kupitia wewe wana Yanga wana matumaini makubwa  ya kusahua vichwa vya dhahabu vya Makambo.Magoli ya kipekee ya akina Mwapee na uonevu wa Hamisi Tambwe kwa makipa wa Ligi kuu.
  Ditram tambua umendikwa mara kumi zaidi ya ulivyo andikwa wakati ulipo ifunga Yanga Hat trick,zaidi ya ulivyo husika kwenye harakati za kuipeleka Stars CHAN.hapa ulipo sasa ni sehemu tofauti kabisa na hapo ulipotoka.Hapa unahitaji kujitoa,utulivu,nidhamu,uvumilivu na usikivu.
  Tambua kuna Mlima mkubwa saana umewekwa mbele yako,shauku ya mshabiki kwa macho na masikio yao yamekaa tayari kutaka kushuhudia  nini utafanya Tarehe Nne.
  Kaa ukijua Hapa ulipo ni Yanga sehemu pekee ambayo kukosea ni mwiko.Mimi ni mdogo wako mshika kalamu nyeusi Mustafa Mtupa Mtoto wa Mkulima na hizi ni Salamu zangu kwako.
  (Mwandshi wa makala haya ni Kalamu nyeusi na unaweza kumpata  @insta,MtotoWamkulima99. @facebook:Mustafa Abainder au nambari ya simu + 255 687 058 966)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: HIZI NI SALAMU ZANGU KWA DITRAM NCHIMBI NA SAFARI YAKE YANGA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top