• HABARI MPYA

  Jumatano, Desemba 18, 2019

  LIVERPOOL YAPIGWA 5-0 NA ASTON VILLA NA KUTUPWA NJE CARABAO

  Jonathan Kodjia akishangilia baada ya kuifungia Aston Villa mabao mawili dakika za 37 na 45 katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Liverpool kwenye mchezo wa Robo Fainali Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao usiku wa jana Uwanja wa Villa Park. Mabao mengine ya Aston Villa yalifungwa na Conor Hourihane dakika ya 14, Morgan Boyes aliyejifunga dakika ya 17 na Wesley Moraes dakika ya 90 na ushei na kuitupa nje Lierpool iliyotumia wachezaji wa timu ya vijana kutokana na kikosi cha kwanza kwenda Qatar kwenye Klabu Bingwa ya Dunia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: LIVERPOOL YAPIGWA 5-0 NA ASTON VILLA NA KUTUPWA NJE CARABAO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top