• HABARI MPYA

    Sunday, December 29, 2019

    TATIZO LA KMC NI KUJIKUNA KWENYE UNYAYO BADALA YA KICHWANI

    Na Mustafa Mtupa, DAR ES SALAAM
    IKIWA ni siku ya Jumatatu tulivu kabisa majira ya saa nne kamili za usiku nikiwa nipo katika moja ya Usafiri wa jumuiya nikiwa natoka kwenye mihangaiko yangu ya kila siku.
    Ilikuwa ni siku ambayo macho yangu yalihisi uzito saana na ilitokana na lepe kubwaa la usingizi kuniandama kichwani mwangu hata likapelekea macho kujihisi uzito usio kifani.
    Sikujua mda gani hasa usingizi ulinipitia lakini ninacho kumbuka ni kuwa wakati usingizi una nipitia nilikuwa nimeweka Headphone masikioni nikiwa nasikiliza moja ya kipindi cha michezo.
    Nikiwa katika usingizi huo mzito huku mwili mzima ukiwa umepumzika lakini Ubongo haukuacha kufanya kazi yake.
    Nikiwa katika hali hiyo ghafla ilinijia taswira ya Klabu ilijizolea umaarufu kwa mda mchache saana hapa nchini.hata ikawafanya watanzania waone ni kawaida kulitaja jina la Klabu hiyo kila lilipowajia.
    Ndani ya msimu mmoja tu ilitosha kuwafanya watoto hawa wa kinondoni kufikia lengo la  kuandikwa kwenye ripoti za makamishna wa michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.
    Miongoni mwa vitu ambavyo KMC walisahau ni sababu ya hayo mafanikio yao waliyokuwa wanayapata hata wakajikita zaidi kwenye kufurahia uwepo wa mafanikio hayo badala ya kujikita zaidi kwenye shughuli ya kulinda chanzo cha chemchem ya mafanikio hayo.
    KMC waliamini kuwa tayari wameshapanda Mlima kilimanjaro Wakati ndo kwanza walikuwa wameuona.waliamini uwepo wa vifaa vya kupandia peke yake bila ya kuwa na muongozaji sahihi wa safari hiyo ya upandaji mlima huo  ingewafanya wafikie tena lengo lao walilowahi kulifikia.
    Kuna mda unaweza kusema kuwa Ubongo wa Etiene Ndairagije bado unawatesa KMC kwani tokea kuondoka kwake hawajapata tena binaadamu mwenye ubongo wenye mawazo pevu  kama yake.
    KMC wana kila kitu cha kupandia mlima lakini bado wanakosa mtu sahihi wa kuwapandisha  mlima huo.kwenye kikosi chao walijaribu kuleta kila miguu iliyo onekana kuwa ina nga'aa kwenye timu nyengine.lakini shida ni kwamba wameshindwa kupata mtu wa kuunganisha miguu hiyo.
    Mafanikio ya Etiene yali waaminisha wanaweza wakaishi nyakati zoote kwa kutegemea vitu walivyonavyo bila ya kujali nani ana viongoza vitu hivyo.
    Ni ukweli usio pingika kuwa KMC walijikuna miguu badala ya kichwa hatimae wakakosa uongozi na kutumbukia gizani.
    Ghafla nikakurupuka kutoka kwenye ndoto hiyo ya kusikitisha ambayo ilinifanya nipate jibu la kuwa tatizo la KMC sio wachezaji bali bado hawajapata  mtu sahihi wa kuwaongoza wachezaji hao.gari nayo ikawa imefika kwenye kituo ninacho shuka na hatimae ikaniacha
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TATIZO LA KMC NI KUJIKUNA KWENYE UNYAYO BADALA YA KICHWANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top