• HABARI MPYA

  Jumatatu, Desemba 16, 2019

  NI LIVERPOOL NA ATLETICO MADRID 16 BORA LIGI YA MABINGWA

  MABINGWA watetezi, Liverpool watamenyana na Atletico Madrid katika hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa, wakati mabingwa wa England, Manchester City watamenyana na Real Madrid. 
  Katika droo iliyopangwa leo Jijini Nyon, Uswisi ikihusisha timu zote nne za Ligi Kuu ya England zilizofuzu kwenye michuano hiyo iliyoanza Agosti, Chelsea itamenyana na Bayern Munich.
  Timu nyingine ya England, Tottenham Hotspur ya kocha Mreno Jose Mourinho itaivaa RB Leipzig inayofundishwa na Julien Nagelsmann
  Borussia Dortmund watamenyana na Paris Saint-Germain, Atalanta watamenyana na Valencia, Lyon na Juventus na Napoli watakutana na Barcelona. 
  Mechi za kwanza za hatua hiyo zitachezwa kati ya February 18, 19, 25 nad 26 na za marudiano zitachezwa kati ya Machi 10, 11, 17 na 18.  


  Ratiba kamili ya hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kupangwa leo mjini Nyon, Uswis 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: NI LIVERPOOL NA ATLETICO MADRID 16 BORA LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top