• HABARI MPYA

    Friday, December 27, 2019

    MSENGI WA KMC ASAINI MIAKA MITATU KUJIUNGA NA STELLENBOSCH YA LIGI KUU AFRIKA KUSINI

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mkabaji chipupizi wa Tanzania, Ally Msengi amesajiliwa na klabu ya Stellenbosch ya Ligi Kuu Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu akitokea Kinondoni Municipal Council (KMC) ya Dar es Salaam.
    Mratibu wa kampuni ya Siyavuma Sports Group, Michael Mwebe ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online leo kwamba Msengi alizivutia klabu kadhaa za Afrika Kusini kabla ya kuamua kumwaga wino Stellenbosch baada ya kocha wa klabu hio kuonesha imani kubwa ya kumpa nafasi katika kikosi chake.
    Msengi ambaye amezichezea timu zote za vijana za taifa kuanzia U17 na 20 anatarajiwa kuanza rasmi maisha mapya Katika Ligi Kuu Afrika Kusini Jumapili ya keshokutwa.
    Kiungo Ally Msengi amesajiliwa na Stellenbosch ya Ligi Kuu Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu

    “Msengi anaanza ukurasa mpya baada ya kufanya vizuri akiwa na klabu ya KMC aliyoichezea kwa takriban msimu mmoja na nusu. Tunaushukuru uongozi wa KMC kwa ushirikiano mkubwa tangu alipotua hapo na pia kumpa baraka zote za kuondoka klabu kwa ajili ya kucheza soka nje ya mipaka ya Tanzania. 
    Siyavuma inaendelea kuamini katika vipaji vya vijana wa Tanzania, Msengi akiwa muendelezo wetu wa kuwapatia fursa ya kucheza soka la nje ya nchi. Ikumbukwe tulianza na Abdi Banda tuliyemtoa Simba na kumpeleka Baroka, baadaye Himid Mao, Eliud Ambokile, Yahya Zaydi na sasa Msengi” amesema Mwebe.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: MSENGI WA KMC ASAINI MIAKA MITATU KUJIUNGA NA STELLENBOSCH YA LIGI KUU AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top