• HABARI MPYA

  Jumanne, Desemba 17, 2019

  UGANDA YAIPIGA BARA 1-0 NA KUTINGA FAINALI CHALLENGE, KUMENYANA NA ERITREA ILIYOICHAPA KENYA 4-1

  Na Mwandishi Wetu, KAMPALA
  NDOTO za Tanzania Bara kutwaa Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kwa mara ya nne zimeyeyuka leo baada ya kuchapwa 1-0 na wenyeji, Uganda katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Lugogo mjini Kampala. 
  Bao lililoizamisha Kilimanjaro Stars inayofundishwa na wachezaji wake wa zamani, Juma Mgunda anayesaidiwa na Zubery Katwila limefungwa na mshambuliaji wa klabu ya Vipers, Fahad Aziz Bayo dakika ya 86 akimalizia krosi ya beki wa kushoto wa KCCA, Mustafa Kizza.
  Sasa Uganda watamenyana na Eritrea kwenye fainali ambao wamewatoa mabingwa watetezi, Kenya kwa kuwachapa 4-1 katika Nusu Fainali ya kwanza leo. Mabao ya Eritrea yalifungwa Oscar Wamalwa aliyejifunga, Abel Solomon, Michael Habte na Robel Kidane. Wamalwa pia aliifungia Kenya bao pekee.

  Ben Ochen wa Uganda akimlamba chenga ya mwili beki wa Tanzania Bara, Bakari Mwamnyeto leo Uwanja wa Lugogo

  Kikosi cha Uganda kilikuwa; Lukwago Charles, Mustafa Kizza, Lwaliwa Halid, John Revita, Anukali Bright/Karim Watambala dk76, Joakim Ojera/Ben Ochen dk56, Fahad Bayo, Joel Madondo, Paul Willa, Shafic Kagimu na Allan Okello.
  Tanzania Bara; Aishi Manula/Metacha Mnata dk13, Juma Abdul, Gardiel Michael, Bakari Mwamyeto, Kelvin Yondani, Jonas Mkunde, Hassan Dilunga, Muzamil Yassin, Ditram Nchimbi, Eleuter Mpepo/Paul Nonga dk90+1, na Nickson Kibabage/Cleophace Mkandala dk88.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UGANDA YAIPIGA BARA 1-0 NA KUTINGA FAINALI CHALLENGE, KUMENYANA NA ERITREA ILIYOICHAPA KENYA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top