• HABARI MPYA

  Jumamosi, Desemba 21, 2019

  YANGA SC YATINGA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP BAADA YA KUIPIGA IRINGA UNITED 4-0

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imefanikiwa kuingia Hatua ya 16 Bora michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 4-0 dhidi ya Iringa United jioni ya leo Uwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.
  Ushindi wa leo wa Yanga umetokana na mabao ya wachezaji wa kigeni watupu, angalau wazawa wawili wakihusika katika usaidizi wa mabao mawili.
  Kiungo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasa ya Kongo (DRC), Papy Kabamba Tshishimbi alifunga bao la kwanza kwa kichwa dakika ya nane akimalizia krosi ya mzawa, kiungo Deus David Kaseke.

  Kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Patrick Sibomana naye akafunga bao la pili dakika ya 10 akimalizia mpira uliowapita mabeki wa Iringa United baada ya krosi ya beki wa kulia, mzawa Cleophas Sospeter Mkandala.
  Beki Mghana Lamine Moro akaifungia Yanga SC bao la tatu kwa kichwa dakika ya 39 akimalizia kona maridad ya Sibomana ambaye pia alimpasia Mkongo mwingine, mshambauliaji David Molinga Ndama ‘Falcao’ kufunga bao la nne dakika ya 70.
  Tatizo la umaliziaji liliwakosesha Yanga SC kuondoka na ‘furushi’ la mabao dhidi ya timu hiyo inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza Tanzana Bara.
  Kikosi cha Yanga SC kilikuwa; Faroukh Shikharo, Cleophas Sospeter/Paul Godfrey dk87, Jaffary Mohamed, Lamine Moro, Ally Mtoni ‘Sonso’, Said Juma ‘Makapu’, Deus Kaseke/Adam Kiondo dk72, Papy Kabamba Tshishimbi/Gustapha Simon dk83, David Molinga, Mrisho Ngassa na Patrick Sibomana. 
  Iringa United; Nelson Emmanuel, Mansour Mussa, Juma Mpeka, Jackson Haule, Geoffrey Albino, Jackson Mahinya, Juma Jega, Msafiri Haji/Salum Upete dk82, Mohamed Mkumba/Dayan Moses Masue dk21, Calvin Jackson/Tensiny Michael dk67 na Kayala Mbutia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YATINGA 16 BORA AZAM SPORTS FEDERATION CUP BAADA YA KUIPIGA IRINGA UNITED 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top