• HABARI MPYA

  Alhamisi, Desemba 19, 2019

  STARS YAAGA MICHUANO YA CHALLENGE KWA KUCHAPWA 2-1 NA HARAMBEE STARS LEO LUGOGO

  Na Mwandshi Wetu, KAMPALA
  TANZANA Bara imeaga michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kwa kuchapwa mabao 2-1 na waliokuwa mabingwa watetezi Kenya jioni ya leo Uwanja wa Lugogo mjini Kampala, Uganda.
  Kenya iliyo chini ya kocha Francis Kimanzi, iliuachia ubingwa wa Challenge baada ya kuchapwa 4-1 na Eritrea juzi ambao leo wanateremka uwanjani kumenyana na wenyeji, Uganda katika fainali.
  Na leo Harambee Stars ikafanikiwa kumalizia hasira zake kwa Kilimanjaro Stars kwa kuwachapa 2-1, mabao ya Kenya yakifungwa na Kenneth Muguna dakika ya 16 akimalizia pasi ya Oscar Wamalwa na Hassan Abdallah dakika ya 36 akimalizia pasi ya Lawrence Juma.

  Nahodha wa Kenya, Joash Onyango akiondoka na mpira mbele ya Eleuter Mpepo wa Tanzania Bara leo Uwanja wa Lugogo

  Na Tanzania Bara chini ya kocha wake, Juma Mgunda ikafanikiwa kupata bao la kufutia machozi dakika ya 82 kupitia kwa beki wake wa kushoto, Gardiel Michael aliyefungwa kwa penalti dakika ya 82 baada ya kiungo Hassan Dilunga kuangushwa.
  Kikosi cha Kenya kilikuwa; Samuel Odhiambo, Joash Onyango, Anthony Wambani, Hassan Abdallah/ Musa Masika dk87, David Owino, Samuel Olwande, Lawrence Juma, Johnstone Omorwa, Moses Mudavadi/ Daniel Sakari dk68, Kenneth Muguna na Oscar Wamalwa.
  Tanzania; David Kisu, Juma Abdul, Gardiel Michael, Bakari Mwamyeto, Kelvin Yondani, Jonas Mkunde/ Baraka Majogoro dk61, Hassan Dilunga, Muzamil Yassin, Ditram Nchimbi, Eleuter Mpepo/ Paul Nonga dk48 na Nickson Kibabage.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: STARS YAAGA MICHUANO YA CHALLENGE KWA KUCHAPWA 2-1 NA HARAMBEE STARS LEO LUGOGO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top