• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 21, 2018

  KMC YAANZA KUWAPA MIKATABA MIPYA WALIOPANDISHA TIMU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC imeendelea kujipanga kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara baada ya kumpa mkataba mpya, mchezaji wake, Rayman Mgungila.
  Meneja wa KMC, Walter Harison ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba Mgungila amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia KMC baada ya kutoa mchango mkubwa msimu uliopita timu ikipanda Ligi Kuu. 
  Mgungila ni mzaliwa wa Magomeni aliyeibukia Friends Rangers chini ya Heri Mzozo pale kabla ya kuchukuliwa na timu ya vijana ya Azam ambako alifikia hadi kucheza timu ya wakubwa na kuwa sehemu ya timu iliyochukua ubingwa wa Tanzania bara mwaka 2013/2014. 

  Rayman Mgungila (kulia), akipeana mkono na Meneja wa KMC FC, Water Harrison baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia klabu hiyo aliyoisaidia kupanda Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu huu

  Na huyo anakuwa mchezaji wa tatu tu kati ya waliopandisha timu kutoka Daraja la Kwanza chini ya kocha Freddy Felix MInziro kupewa mkataba mpya, baada ya viungo Abdulhalim Humud na Adam Kingwande waliowahi kuchezea klabu ya Simba.
  KMC pia imesajili wachezaji wanne wapya ambao ni kiungo mshambuliaji, Abdul Hillary Hassan kutoka Tusker FC ya Kenya, kipa Juma kaseja na mabeki Aaron Lulambo, Sadallah Lipangile na Ali Ali.
  Tayari Minziro amekwishaondolewa na nafasi yake imechukuliwa na Mrundi Ettienne Ndayiragijje ambaye misimu miwili iliyopita alikuwa Mbao FC ya Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC YAANZA KUWAPA MIKATABA MIPYA WALIOPANDISHA TIMU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top