• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 28, 2018

  MBEYA CITY YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MOROGORO…ALLIANCE YAIADHIBU BIASHARA UNITED RORYA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Mbeya City leo imeichapa mabao 2-1 Mtibwa Sugar katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. 
  Baada ya dakika 45 ngumu za kipindi cha kwanza timu hizo zikimaliza bila kufungana, hatimaye kipindi cha pili mambo yakabadilika na wageni wakapata mabao yao.
  Na sifa ziwaendee wafungaji wa mabao hayo, Mohammed Chuga dakika ya 61 na Mohamed Kapeta dakika ya 77 kwa upande wa Mbeya City na Issa Kajia aliyewafungia wenyeji, Mtibwa.

  Mbeya City walipokuwa wakipasha misuli moto kabla ya mchezo wa leo  

  Mchezo huo ulikuwa maalum kwa timu zote kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Agosti 22.
  Katika mchezo mwingine wa kujiandaa na Ligi Kuu leo, timu ya Alliance Schools ya Mwanza imewafunga wageni wenzao wa Ligi Kuu, Biashara United ya Mara 1-0 Uwanja wa Obwere mjini Shirati wilayani Rorya mkoani Mara.
  Huo ni mchezo wa pili wa kujipima nguvu baina ya timu hizo, baada ya Biashara United kushinda 4-2 kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Nyamagana mjini Mwanza wiki mbili zilizopita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MBEYA CITY YAICHAPA MTIBWA SUGAR 2-0 MOROGORO…ALLIANCE YAIADHIBU BIASHARA UNITED RORYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top