• HABARI MPYA

    Friday, July 27, 2018

    PAZIA LA USAJILI; YANGA WAFANYA MAAJABU DAKIKA ZA MWISHO, SIMBA YAMBAKIZA NDEMLA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    DIRISHA la usajili limefungwa Alhamisi ya Julai 26, kwa klabu za Simba na Yanga kufanya usajili wa dakika za mwishoni.
    Simba SC imefanikiwa kumbakiza kiungo wake, Said Hamisi Ndemla aliyekuwa anawaniwa na AFC Eskilstuna ya Sweden – lakini pia imekamilisha usajili wa kiungo mpya, Hassan Dilunga kutoka Mtibwa Sugar ya Morogoro. 
    Wawili hao kwa pamoja na wachezaji wengine watatu, Erasto Nyoni, Meddie Kagere na Haruna Niyonzima wamekwenda kuungana na wenzao kambini nchini Uturuki baada ya kusaini mikataba yao.
    Kipa Klaus Nkinzi Kindoki kutoka DRC (kulia) akikabidhiwa jezi na Meneja w aYanga, Hafidh Saleh
    Geoffrey Mwashiuya akifurajia na jei ya Singida Unioted baada ya kusiani mkataba w miaka miwili kutoka Yanga SC


    Yanga SC imefanikiwa kumbakiza beki wake tegemeo, mkongwe Kelvin Yondan, lakini imenasa saini za wachezaji wawili kutoka DRC kipa Klaus Nkinzi Kindoki na mshambuliaji Heritier Makambo, ambaop kila mmoja kusaini mkataba wa miaka miwili.
    Wachezaji hao walikuwa kwenye majaribio Yanga kwa wiki kadhaa chini ya kocha Mwinyi Zahera wa Yanga SC, Mkongo mwenzao pia.
    Lakini pia Yanga imempoteza beki wake wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy aliyehamia Nkana FC ya Zambia, huku jaribio la kuwapeleka kwa mkopo baadhi ya wachezaji wake, akiwemo kipa Youthe Rostand likikwama dakika za mwishoni. 
    Azam FC imemsajili mshambuliaji Daniel Lyanga kutoka Singida United alikocheza kwa muda mfupi tu akitokea Fanja SC ya Oman, ambayo ilimnunua Simba SC mwaka juzi.
    Singida imeziba pengo la Lyanga kwa kuwasajili winga Geoffrey Mwashiuya kutoka Yanga na mshambuliaji Mghana, Hans Kwofie akitokea Smouha S.C ya Misri kila mmoja akisaini mkataba wa miaka miwili.

    Beki na Nahodha, Kevin Yondan akisaini mkataba wa kubaki Yanga jana

    Hadi Alhamisi jioni, TFF ilisema ni klabu moja tu, African Lyon ilikuwa haijakamilisha usajili, lakini Bin Zubeiry Sports – Online imezungumza na Rais wa klabu hiyo, Rahim Kangenzi ‘Zamunda’ ambaye amesema kwamba wamekamilisha usajili wao ndani ya muda.
    “Usajili una muda wake maalum wa mwisho, na sisi tuliuzingatia kuhakikisha tunasajili kulingana na taratibu. Tunashukuru, suala la usajili kwetu limepita na limekwenda vizuri,”alisema, Zamunda.   
    TFF inatarajiwa kutoa ripoti kamili Ijumaa mchana juu ya namna zoezi lilivyokwenda hadi kukamilika kwake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAZIA LA USAJILI; YANGA WAFANYA MAAJABU DAKIKA ZA MWISHO, SIMBA YAMBAKIZA NDEMLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top