• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 25, 2018

  MAREFA WA MAURITIUS KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA GOR MAHIA JUMAPILI TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAREFA kutoka Mauritius ndiyo watachezesha mechi ya Kundi D, Kombe la Shirikisho Afrika kati ya wenyeji, Yanga SC na Gor Mahia FC ya Kenya Jumapili kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Hao ni Ahmad Imtehaz Heeralall atakayepuliza filimbi akisaidiwa na Cauvelet Louis Ralph Fabien na Akhtar Nawaz Rossaye washika vibendera.
  Yanga haijashinda mechi hata moja kati ya tatu za awali, ikifungwa mbili zote 4-0, ya kwanza dhidi ya MC Alger nchini Algeria Mei 6 na ya pili dhidi ya Gor Mahia Julai 18 mjini Nairobi wakati nyingine walitoka sare ya 0-0 na Rayon Sport mjini Dar es Salaam Mei 16. 

  Baada ya mechi na Gor Jumapili, Yanga wataikaribisha USM Alger Agosti 19 kabla ya kwenda kukamilisha mechi zake za kundi hilo kwa kumenyana na wenyeji, Rayon Sport Agosti 28.
  Habari njema kuelekea mchezo huo ni wachezaji wawili, kiungo Deus Kaseke na mshambuliaji Matheo Anthony kupatiwa leseni na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kucheza mechi hizo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAREFA WA MAURITIUS KUCHEZESHA MECHI YA YANGA NA GOR MAHIA JUMAPILI TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top