• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 25, 2018

  KILIMANJARO QUEENS YAENDELEA KUJIFUA KWA MCHEZO WA MWISHO CHALLENGE

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens leo imeendelea na mazoezi yake ya kujiandaa na mchezo wake wa mwisho wa mashindano ya CECAFA kwa Wanawake dhidi ya Ethiopia.
  Mchezo huo dhidi ya Ethiopia utachezwa Ijumaa Julai 27,2018 Stade de Kigali saa 8 mchana ambayo ni saa 9 alasiri kwa nyumbani Tanzania.
  Kwenye mazoezi ya leo yaliyofanyika kwenye viwanja vya Shirikisho la Mpira wa Miguu la Rwanda(FERWAFA) golikipa Fatuma Omary aliyekuwa majeruhi amerejea kikosini na ameshiriki mazoezi yote mwanzo mpaka mwisho.
  Mchezaji pekee ambaye hakushiriki mazoezi hayo kwasababu ya majeruhi ni Maimuna Khamis.

  Kilimanjaro Queens itaendelea na mazoezi yake kesho asubuhi kwenye viwanja vya IPRC,Kicukiro.
  Timu hiyo ya Tanzania Bara ina alama 4 baada ya kucheza mechi 3 ikifungwa mchezo mmoja na Rwanda kwa bao 1-0,kabla ya kutoka sare ya bao 1-1 na Kenya mchezo wa pili na kuifumua Uganda kwa mabao 4-1 kwenye mchezo wa 3.
  Kili Queens inakamata nafasi ya pili nyuma ya Uganda yenye alama 6 kabla ya mechi za leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS YAENDELEA KUJIFUA KWA MCHEZO WA MWISHO CHALLENGE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top