• HABARI MPYA

  Jumatatu, Julai 30, 2018

  BIASHARA UNITED YA MARA YAENDA KENYA KWA MECHI ZAIDI ZA KUJIANDAA NA LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, MARA
  KLABU ya Biashara United ya Mara inatarajiwa kuondoka wiki hii kwenda Kenya kwa ziara ya mechi kadhaa za kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Hiyo ni baada ya timu mpya katika Ligi Kuu kumaliza mechi zake za kujipima nguvu kutazama uimara wa kikosi chake wilaya za Rorya na Tarime mkoani Mara.
  Mchezo wa kwanza wa timu hiyo dhidi ya timu ya Rorya Combine ulifanyika katika Uwanja wa Nyamagaro na Biashara United kufanikiwa kushinda mabao matatu kwa bila.
  Siku iliyofuata (28/7/2018) timu hiyo ilitakiwa kucheza na timu ya Mbao Fc ambapo hata hivyo timu hiyo ya Mbao Fc hakufika na hivyo kulazimika kucheza na timu ya Alliance ya jijini Mwanza na kupoteza mchezo huo baada kufungwa bao moja kwa bila mchezo uliochezwa kwa dakika 70.

  Julai 29/7.2018 TIMU ya Biashara United Mara iliwaalika tena timu ya Alliance kutoka jijini Mwanza katika Uwanja wa KRA Sirari ambapo Alliance walifanikiwa kushinda mabao mawili kwa bila.
  Meneja wa timu hiyo Aman Josiah amesema michezo hiyo imesaidia kujua uimara na udhaifu wa timu hiyo na kusema bado timu hy inahtaji michezo zaidi ya kujipima nguvu.
   "Mimi nadhani michezo hii itatusaidia sana kuangali uimara na udhaifu wa kikosi chetu kabla ya kuanza kwa ligi kuu hapo August 22" alisema Aman.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BIASHARA UNITED YA MARA YAENDA KENYA KWA MECHI ZAIDI ZA KUJIANDAA NA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top