• HABARI MPYA

  Ijumaa, Julai 27, 2018

  MALCOM ATAKA KUWA SHUJAA MPYA MBRAZIL BARCELONA

  WINGA mpya wa Barcelona, Malcom Filipe Silva de Oliveira maarufu tu kama Malcom, amesema kwamba anataka kuendeleza kazi nzuri iliyofanywa na wachezaji wa Kibrazil ndani ya Barcelona.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 amesema hayo baada ya kutambulishwa katika kambi ya timu nchini Marekani, kufuatia kukamilisha uhamisho wake wa utata kujiunga na wababe hao wa La Liga mapema wiki hii kwa dau la Pauni Milioni 45, licha ya Roma nayo kutangaza imefikia makubaliano na Bordeaux ya kununua saini ya nyota huyo.
  Akizungumza wakati wa utambulisho wake, makao makuu ya Nike mjini Portland, Malcom alisem; “Najua ni changamoto kuchezea FC Barcelona, lakini hii ni ndoto niliyokuwa tangu nilipokuwa mdogo. Mimi ni mshambuliaji, na mwenye uwezo mkubwa wa kukabiliana na mchezaji ana kwa ana, nina kasi sana, na ninasaidia ulinzi,”amesema.

  Malcom (kulia) anataka kuwa shujaa mpya Mbrazil ndani ya kikosi cha Barcelona

  “Nilipokuwa mdogo, nilikuwa navutiwa na Ronaldinho. Neymar pia. Natumai kufuata nyayo zao wote wachezaji wakubwa wa Brazilian waliotamba Barca,”. 
  Malcom pia amesema kwamba alikuwa anapenda kucheza pamoja na Lionel Messi, akimuita mshambuliaji huyo wa Barcelona ni gwiji, na anatumai atajifunza mengi kutoka kwake.
  Malcom alitambulishwa Alhamisi mjini Beaverton, Oregon – ambako Barca imeweka kambi Marekani ikishiriki michuano ya Kombe la Mabingwa wa Kimataifa kujiandaa na msimu – na Rais wa klabu, Josep Maria Bartomeu, Mkurugenzi wa Usajili, Eric Abidal na Makamu wa Rais, Jordi Mestre.
  Ni Abidal ndiye aliyempigia simu Rais wa Bordeaux, Stephane Martin na kuwaambia klabu hiyo ya Ufaransa kwamba, Barca inaweza kutoa fedha zaidi ya wanazotaka kutoa Roma kumnunua nyota huyo chipukizi.
  Klabu hiyo ya Serie A inasemekana ilikuwa imekwishakamilisha dili hilo na Bordeaux kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 wa Kibrazil, winga Malcom – kiasi cha kufikia kuthibitishia dili hilo kwenye Twitter, na mashabiki wa Roma walikuwa tayari Uwanja wa Ndege kusubiri kumpokea mchezaji huyo. 
  Pamoja na hayo, Saa 5:00 Barca wakakamilisha uhamisho wa mchezaji huyo kwa dau la Pauni Milioni 45 na kusababisha ofa ya Roma kutupiliwa mbali, na Malcom akabadilisha ndege kwenda Marekani badala ya Rome.
  Hii ilimkasirisha sana Rais wa Roma, Jim Pallotta na kusema Barca wamefanya mambo ya ‘kihuni nakinyume cha maadili’ alipohojiwa na Radio Alhamisi na kuwalaani Bordeaux kwa walichokifanya.
  “Barcelona wameomba radhi juu ya walichokifanya na namna walivyofanya. Sikubaliani kabisa na ombi lao la msamaha. Namna pekee ninaweza kukubali ombi la msamaha wa Barca ni kumleta mchezaji kwetu, wakimleta mchezaji kwetu, hilo haliwezi kutokea. Labda pia wakituletea Messi,”.' 
  Barca ilihamishia nguvu zake za kifedha katika kumsajili Malcom, baada ya ofa yao ya Pauni Milioni 65 kumsajili kiungo wa Chelsea, Willian kupigwa chini. Hivyo wakaenda klumpelekea jezi namba 7 Malcom ambaye sasa ataanza kuchezea timu yake mpya Jumapili katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Tottenham Hotspur mjini Los Angeles.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MALCOM ATAKA KUWA SHUJAA MPYA MBRAZIL BARCELONA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top