• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 24, 2018

  MZIMBABWE ELISHA MUROIWA ATUA YANGA KWA MSAADA KUTOKA SINGIDA UNITED

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Singida United imeendelea kuimarisha uhusiano wake na vigogo, Yanga SC baada ya kuwapa mchezaji mwingine, beki wa kulia Elisha Muroiwa.
  Katibu Mkuu, Abdulrahman Sima kwenda TFF amesema katika barua yake aliyowaandikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwamba wameagizwa na Mlezi wa timu, Mheshimiwa Dk. Mwigulu Nchemba, Mbunge wa Iramba Magharibi awape Yanga mchezaji huyo.
  “Dk Mwigulu amesema hakuna mgogoro wa kiusajili kwani alitoa ridhaa kwa mchezaji kwenda kujisajili na alikubaliana na viongozi wa Yanga wafanye na kwamba hakuna fedha inayorudishwa bali usajili huo ni mchango wake kwa klabu kwa makubaliano kwamba kama mchezaji hatakuwa na kiwango cha kubaki Yanga ataletwa Singida United,”amesema Sima.  

  Beki Elisha Muroiwa ametua Yanga kwa msaada kutoka Singida United  

  “Tumekwishamlipa (Muroiwa) fedha zake za mkataba, hatudai huu ni mwendelezo wangu wa kuwasaidia Yanga nikiwa ni mdau wa mpira wa miguu. Na siyo kuwasaida Yanga, tu hata timu nyingine inapohitajika msaada wangu nitazisaidia kama nitakuwa na uwezo wa kuzisaidia,” Sima amemnukuu Mheshimiwa Nchemba katika maelezo yake.
  Muroiwa anakuwa mchezaji wa tatu Yanga wanapewa na Singida United baada ya Feisal Salum ‘Fei Toto’ na Deus Kaseke, wote viungo. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MZIMBABWE ELISHA MUROIWA ATUA YANGA KWA MSAADA KUTOKA SINGIDA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top