• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 21, 2018

  KILIMANJARO QUEENS WAENDELEA KUSUASUA KOMBE LA CHALLENGE WANAWAKE...LEO WAMETOA SARE NA KENYA

  Na Mwandishi Wetu, KIGALI
  TIMU ya wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens imeendelea kufanya vibaya kwenye michuano ya Kombe la Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Challenge baada ya leo kulazimishwa sare ya 1-1 na Kenya Uwanja wa Nyamirambo mjini Kigali. 
  Katika mchezo huo uliofanyika jioni, bao la Kili Queen inayofundishwa na kocha Bakari Shime limefungwa na Donisia Daniel wakati la Kenya limefungwa na Mwanalima Adam Jereko.
  Hali ni mbaya kwa Twiga Stars, mabingwa watetezi baada ya mechi bila ushindi, kufuatia kuchapwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza na wenyeji, Rwanda bao pekee la Kalimba Alice dakika ya 34.  Sasa Kili Queens italazimika kushinda dhidi ya Uganda na Ethiopia kwenye mechi zake zijazo kuangalia uwezekano wa kutetea taji ililolitwaa mjini Kampala mwaka jana. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KILIMANJARO QUEENS WAENDELEA KUSUASUA KOMBE LA CHALLENGE WANAWAKE...LEO WAMETOA SARE NA KENYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top