• HABARI MPYA

  Jumanne, Julai 24, 2018

  SIMBA SC YAWATEMA NDUNDA, SHOMARI, MAVUGO, JUUKO NA MWAMBELEKO

  Na Sada Salim, DAR ES SALAAM
  SIMBA SC inawatafutia timu za kuchezea kwa mkopo wachezaji wake watano, akiwemo kipa Said Mohammed Ndunda kutokana na kile kilichoelezwa kutokuwa na nafasi kwenye kikosi cha sasa.
  Pamoja na Ndunda, wengine ni kipa Emmanuel Mseja, beki Ally Shomari, kiungo Jamal Mwambeleko na mshambuliaji Moses Kitandu ambao wote hawajasafiri na timu kwenda Uturuki kwenye kambi ya kujiandaa na msimu mpya.
  Wachezaji waliopo na Simba SC kambini mjini Instanbul, Kaskazini Mashariki mwa Uturuki ni makipa Deo Munishi ‘Dida’, Aishi Manula, Ally Salim mabeki Shomari Kapombe, Serge Wawa, Yussuf Mlipili, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Paul Bukaba, viungo Mohammed Ibrahim ‘Mo’, Rashid Juma, James Kotei, Muzamil Yassin, Jonas Mkude, Cletus Chama na Shiza Kichuya, washambuliaji Marcel Kaheza,  Abdul Hamisi, Emmanuel Okwi, Nahodha John Bocco, Adam Salamba na Mohammed Rashid.

  Said Mohammed Ndunda anatolewa kwa mkopo kwa sababu hana tena nafasi kwenye kikosi cha sasa Simba

  Beki Erasto Nyoni wanatarajiwa kuondoka usiku wa kuamkia kesho pamoja na Wanyarwanda Haruna Niyonzima na Meddie Kagere. Nyoni alikuwa ana matatizo ya kifamilia, wakati Niyonzima na Kagere walichelewa kupata visa.
  Kiungo Said Ndemla hajasafiri na timu kwa sababu yupo kwenye mipango ya kujiunga na klabu ya AFC Eskilstuna ya Sweden akiwa amemaliza mkataba wake Simba.
  Mshambulaji Mrundi, Laudit Mavugo ameachwa wakati beki Mganda, Juuko Murshid ameruhusiwa kwenda kutafuta timu nyingine. 
  Simba SC imefikia katika hoteli ya Reen Park & Resorts mjini Istanbul na inafanya mazoezi kwenye moja ya viwanja vitano vilivyopo kwenye hoteli hiyo.
  Wachezaji wa Simba SC wakifurahia katika kambi yao ya Uturuki
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAWATEMA NDUNDA, SHOMARI, MAVUGO, JUUKO NA MWAMBELEKO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top