• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 22, 2018

  KMC WAMSAJILI JAMES, MDOGO WAKE SIMON MSUVA ALIYEWIKA MBAO FC MSIMU ULIOPITA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC imefanikiwa kumsajili mshambuliaji, James Msuva kutoka klabu ya Mbao FC ya Mwanza kwa mkataba wa mwaka mmoja.
  Meneja wa KMC, Walter Harison ameiambia Bin Zubeiry Sports – Online kwamba Msuva aliyewahi kuchezea timu za vijana za Simba na Yanga, amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuhamishia huduma zake KMC baada ya kazi nzuri akiwa na Mbao FC msimu uliopita. 
  Harrison amesema kwamba wanatarajia Msuva atakuwa na mchango mkubwa kwa timu hiyo kufanya vizuri msimu ujao kutokana na uwezo wake mkubwa aliouonyesha katika Ligi Kuu akiwa na Mbao FC msimu uliopita

  James Msuva (kulia) na Meneja wa KMC, Walter Harrison baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja

  Msuva anakuwa mchezaji wa tano kusajiliwa KMC pia baada ya kiungo mshambuliaji, Abdul Hillary Hassan kutoka Tusker FC ya Kenya, kipa Juma kaseja na mabeki Aaron Lulambo, Sadallah Lipangile na Ali Ali.
  Hadi sasa ni wachezaji watatu tu nwaliokuwemo kwenye kikosi kilichopandisha timu kutoka Daraja la Kwanza chini ya kocha Freddy Felix Minziro ambao wamepewa mkataba mpya, viungo Rayman Mgungila aliyewahi kuchezea Azam FC, Abdulhalim Humud na Adam Kingwande waliowahi kuchezea klabu ya Simba.
  Tayari Minziro amekwishaondolewa na nafasi yake imechukuliwa na Mrundi Ettienne Ndayiragijje ambaye misimu miwili iliyopita alikuwa Mbao FC ya Mwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KMC WAMSAJILI JAMES, MDOGO WAKE SIMON MSUVA ALIYEWIKA MBAO FC MSIMU ULIOPITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top