• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 25, 2018

  TENGA AWAASA TFF KUFIKIRIA UPYA KUONGEZA IDADI YA WACHEZAJ WA KIGENI LIGI KUU

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Bodi ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Leodegar Tenga ameliomba Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kupitia upya na kwa kina sheria ya wachezaji 10 wa kigeni katika timu za Ligi Kuu.
  Sheria hiyo iliyopitishwa hivi karibuni na TFF, inaruhusu timu zinazoshiriki Ligi Kuu nchini kusajili wachezaji wa kigeni 10 kutoka idadi ya awali iliyoruhusu timu inayoshiriki ligi kuu kuwa na wachezaji wakigeni saba.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari mjini Dar es Salaam leo, Tenga amesema sheria hii ikiwezekana ipitiwe tena kwa kina ili ionekane kama inaweza kusaidia ligi hiyo.

  Mwenyekiti wa BMT, Leodegar Tenga ameiomba TFF kupitia upya sheria ya wachezaji 10 wa kigeni Ligi Kuu 

  “Kuwe na tathimini ya kina juu ya sheria hii tujiulize kama kweli inaweza kusaidia timu zetu na wachezaji wa hapa nyumbani pia tutafakari kama tunaweza kufika tunapokwenda kwa sheria hii.
  “Wakati mwingine kuwa na ushirikishwaji mzuri ili watu watoe maoni yao juu ya hili jambo na hata tunaposajili wachezaji hawa tuhakikishe tunasajili wachezaji wenye viwango vizuri,” amesema Tenga.
  Aidha, katika mkutano huo mwenyekiti huyo amesisitiza vyama vya michezo kitaifa kuhakikisha vinafuata sheria za kimichezo vizuri na kuhakikisha kunakua hakuna migogoro ya muda mrefu  kwenye vyama.
  TFF imeongeza idadi ya wachezaji wa kigeni katika Ligi Kuu saba hadi 10 kuanzia msimu ujao. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TENGA AWAASA TFF KUFIKIRIA UPYA KUONGEZA IDADI YA WACHEZAJ WA KIGENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top