• HABARI MPYA

  Jumamosi, Julai 28, 2018

  SIMBA SC KUMENYANA NA MC OUJDA YA LIGI KUU YA MOROCCO JUMATANO MJINI ISTANBUL

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
  TIMU ya Simba SC inatarajiwa kuwa na mchezo wa kirafiki na Mouloudia Club of Oujda ya Morocco Jumatano wiki ijayo Uwanja wa Kartepe Green Park mjini Istanbul kuanzia Saa 10:00 kwa saa Saa 12:00 jioni kwa saa za Afrika Mashariki.
  Msemaji wa Simba SC, Hajji Sunday Manara amesema kwamba MC Oujda inayoshiriki Ligi Kuu ya Morocco, maarufu kama Botola nayo kambini nchini Uturuki kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Manara amesema ni mchezaji mmoja tu ambaye hayupo kambini nchini Uturuki naye ni kiungo Haruna Niyonzima ambaye ametoa udhuru wa matatizo ya kifamilia, lakini anatarajiwa kuwa Dar es Salaam mapema wiki ijayo.
  Na atakaporejea, Niyonzima anayeingia msimu wa pili Simba SC tangu asajiliwe kutoka Yanga SC atasafiri pia kwenda kambini Uturuki.

  Mmoja kati ya wachezaji wapya wa Simba SC msimu huu, Hassan Dilunga akiwa mazoezini Uturuki

  Kikosi kamili cha Simba SC kilichopo kambini katika hoteli ya Reen Park & Resorts mjini Istanbul kinaundwa na makipa; Aishi Manula, Deogratius Munishi ‘Dida’ na Ally Salim.
  Mabeki ni Shomali Kapombe, Asante Kwasi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Nicholas Gyan, Pascal Wawa, Erasto Nyoni, Yussuf Mlipili, Paul Bukaba, Vincent Costa na Salim Mbonde. 
  Viungo ni James Kotei, Jonas Mkude, Muzamil Yaasin, Shiza Kichuya, Cletus Chama, Haruna Nionzima, Hassan Dilunga, Mohammed ‘Mo’ Ibrahim, Marcel Kaheza, Abdul Hamisi, Rashid Juma na Said Ndemla.
  Washambuliaji ni Emmanuel Okwi, John Bocco, Meddie Kagere, Adam Salamba na Mohammed Rashid.
  Simba SC imeweka kambi huko kwa maandalizi ya msimu mpya ikiwa chini ya kocha wake mpya, Mbelgiji Patrick J Aussems anayesaidiwa na Mrundi, Masoud Juma, Mtunisia Adel Zrena Kocha wa mazoezi ya utimamu wa mwili na Muharami Mohammed ‘Shilton’ kocha wa makipa.
  Kikosi kinatarajiwa kurejea nchini Agosti 6 tayari kwa tamasha la kila mwaka la klabu, Simba Day ambalo hufanyika Agosti 8 Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC KUMENYANA NA MC OUJDA YA LIGI KUU YA MOROCCO JUMATANO MJINI ISTANBUL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top