• HABARI MPYA

    Friday, July 20, 2018

    SHIZA RAMADHANI KICHUYA YUKO TAYARI KWA MSIMU MPYA SIMBA SC

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    WINGA machachari wa Simba SC, Shiza Ramadhani Kichuya yuko tayari kwa msimu wa tatu Simba SC akiwa na malengo ya kufanya vizuri zaidi.
    Kichuya aliyejiunga na Simba SC mwaka juzi akitokea Mtibwa Sugar amejiunga na kikosi cha timu hiyo tayari kwa safari ya Uturuki Jumamosi usiku.
    Kichuya amejiunga na timu hiyo baada ya mazoezi yake binafsi ya awali kujiweka fiti kufuatia mapumziko ya mwezi mzima baada ya msimu mzuri uliopita.
    Shiza Kichuya akiwa gym baada ya kufanya mazoezi ya kutosha 

    Kichya aliisaidia Simba SC kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa mara ya kwanza baada ya miaka mitano.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHIZA RAMADHANI KICHUYA YUKO TAYARI KWA MSIMU MPYA SIMBA SC Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top