• HABARI MPYA

  Jumapili, Julai 29, 2018

  YAHYA ZAYED AREJEA KIKOSINI AZAM FC BAADA YA KUSHINDWA MAJARIBIO AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Azam FC, Yahya Zayed amerejea mjini Dar es Salaam kutoka Afrika Kusini alipokwenda kufanya majaribio ya kujiunga na klabu ya Bidvest Wits ya huko.
  Taarifa kutoka Afrika Kusini zinasema kwamba Bidvest haikuvutiwa na Zayed baada ya kumtazama kwa takriban wiki moja na kumruhusu kurejea nyumbani kuendelea kupata uzoefu kabla ya kumuita tena baadaye.
  Zayed aliondoka nchini akiwa tayari amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia Azam FC – hivyo yumo kwenye kikosi timu hiyo kwa ajili ya msimu wa Ligi Kuu unaotarajiwa kuanza Agosti 22.

  Yahya Zayed anarejea Azam FC baada ya kushindwa majaribio  Bidvest Wits 

  Zayed alikuwemo kwenye kikosi kilichoisaidia Azam FC kutwaa taji la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame mapema mwezi huu.
  Azam FC iliichapa Simba SC mabao 2-1 na kubeba Kombe la Kagame Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam Julai 13, mwaka huu hiyo ikiwa ni mara ya pili kwao kutwaa taji hilo baada ya mwaka 2015.
  Mchezaji mwingine kwenye kikosi cha Azam FC kilichotwaa Kombe la Kagame, mshambuliaji pia, Shaaban Iddi Chilunda amechukuliwa kwa mkopo na Tenerife ya Daraja la Kwanza Hispania. Amekwenda kuungana na mchezaji mwingine wa zamani wa Azam FC katika kikosi hicho, Farid Mussa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YAHYA ZAYED AREJEA KIKOSINI AZAM FC BAADA YA KUSHINDWA MAJARIBIO AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top