• HABARI MPYA

  Jumatano, Julai 25, 2018

  MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA TFF DHIDI YA KESI YA WAMBURA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imekataa maombi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kutaka kesi iliyofunguliwa na Makamu wa Rais wa Shirikisho hilo, Michael Wambura ifutwe.
  Wambura alifungua kesi kupinga hukumu ya Kamati ya Maadili na Rufaa ya za TFF zilizomfungia maisha kujihusiaha na soka, hivyo kumuonfoa madarakani.
  Wambura alifungua kesi hiyo Namba 11 ya mwaka 2018, mahakamani hapo akipinga adhabu hiyo ambayo ilitolewa Aprili 6, mwaka huu ambapo TFF iliweka pingamizi ikiitaka mahakama kuifuta kesi hiyo kwa kuwa mlalamikaji alikuwa hajapitia ngazi nyingine za kimaamuzi kwenye soka.

  Michael Wambura ameipa pigo la kwanza TFF mahakamani leo

  Katika pingamizi hilo, TFF ilidai kuwa Wambura alipaswa kukata rufaa katika ngazi zingine za soka ikiwamo Shirikisho la Soka Afrika (CAF), na baadaye Mahakama ya Usuluhishi ya Michezo (CAS) kabla ya kwenda Mahakama za kawaida.
  Akitoa uamuzi huo jana, Jaji Wilfred Dyabsobera, amesema mahakama imetupilia mbali pingamizi na hoja za TFF na kutaka kesi ya msingi iendelee.
  Jaji, Dyabsobera katika hukumu yake aliona kwamba hoja hizo za TFF zinapingana na Katiba na Kanuni za TFF pamoja na sheria mbalimbali za nchi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MAHAKAMA YATUPILIA MBALI PINGAMIZI LA TFF DHIDI YA KESI YA WAMBURA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top